Alumniportal Deutschland

Alumniportal Deutschland
Foto: Alumniportal Deutschland
Makumi elfu ya watu kutoka sehemu zote duniani wanasoma, wanafanya kazi au wanafanya utafiti nchini Ujerumani au kwenye taasisi za Kijeruma nchi za nje au wanashiriki mafunzo ya elimu ya juu au kozi za lugha. Alumniportal Deutschland, jukwaa la njia ya mtandao la watu walioishi au kusoma Ujerumani linaweza kuwasaida kuwa pamoja katika mawasiliano baina yao na nchi ya Ujerumani pindi wanaporejea kwenye nchi zao.

Jukwaa la Alumniportal Deutschland lipo kwenye mtandao wa intaneti toka Septemba 2008. Lango hili la mtandaoni ni jukwaa la mawasiliano kwa jumuiya ya watu wote duniani waliowahi kusoma au kufanya kazi Ujerumani wenye taaluma zinazokaribiana, ujuzi na kuvutiwa binafsi na mambo ya Ujerumani limeanzishwa. Kiini cha jukwaa hili mawasiliano kupitia intaneti, ambapo watu hao huanzisha, hutunza na kuendeleza mawasiliano, wakibadilishana mawazo katika vikundi, vijukwaa na blogu na wakishiriki pia kwenye semina kwa njia ya intaneti. Jarida hutoa mada anuai za kuvutia, fursa za ajira, dondoo na taarifa kuhusu lugha ya Kijerumani pamoja na taarifa na habari zinawahusu.

Alumniportal Deutschland si kwa ajili ya wale waliopata ufadhili kamili kutoka kwenye taasisi bali ipo wazi hata kwa wale waliojigharamia wao wenyewe mafunzo yao nchini Ujerumani au katika taasisi za Kijerumani nje ya nchi Hii ina maana kuwa ni jukwaa la kwanza la wote waliowahi kusoma au kufanya kazi nchini Ujerumani kutoka dunia nzima. Tunakukaribisha ujiunge na Alumniportal Deutschland, utengeneze wasifu wako, uendelee kuwasiliana na Ujerumani huku ukitanua mtandao wako duniani!

Alumniportal Deutschland ni huduma inayotolewa bila kulipia chini ya udhamini Wizara ya mambo ya Nje ya Ujerumani kupitia mashirika matatu ya Kijerumani yenye uzoefu wa miaka mingi katika nyanja za utamaduni wa kigeni na sera za elimu. Goethe-Institut ni miongoni mwa mashirika matatu, mchango wake ukiwa kwenye mada za "utamaduni" na "lugha ya Kijerumani" na huduma kwa waliowahi kupita katika taasisi hiyo.

Juu