Mpango wa PASCH
Shule: Washirika kwa Ajili ya Kesho

Kuchochea hamasa kuhusu Ujerumani, kuwahamasisha vijana kujifunza Kijerumani na kuwaunganisha kimataifa - haya ndiyo malengo ya Mpango wa PASCH wa “Shule: Washirika kwa Ajili ya Kesho”.

Wanafunzi wa shule za PASCH wanatabasamu. Wameinua maneno tofauti ya Kijerumani kwenye karatasi za rangi. © PASCH-net/Anne Essel

Misingi ya Mwongozo

Misingi minne ya mwongozo inatoa mwelekeo wa PASCH:
  • fursa kupitia elimu
  • kupanua upeo kwa kutumia lugha nyingi
  • upatikanaji wa lugha na elimu
  • kushughulikia changamoto za baadaye kwa pamoja kama jumuiya ya kimataifa ya wanafunzi

Kujifunza. Pamoja. Duniani kote!

Ikiwa na jukumu muhimu katika Mpango wa PASCH, Goethe-Institut hufanya jitihada ya kuibua hamasa ya kujifunza lugha ya Kijerumani. Lengo ni Kijerumani kuwa sehemu ya kudumu na ya muda mrefu ya mtaala wa shule zote za PASCH.

Hivyo, wataalamu wa lugha ya Kijerumani hufanya kazi moja kwa moja katika matawi mengi ya Goethe-Institut duniani na kutoa ushauri kwa shule zinazotaka kuanza au kuendeleza ufundishaji wa Kijerumani kama lugha ya kigeni. Aidha, Goethe-Institut huzipa shule za PASCH vifaa vya kisasa vya kufundishia Kijerumani kama lugha ya kigeni.

Walimu wa Kijerumani katika shule za PASCH wanastahiki kupata mafunzo ya mbinu na maarifa pamoja na kozi za lugha zinazotolewa na Goethe-Institut. Baadhi ya wanafunzi huchaguliwa kila mwaka kushiriki katika kambi za vijana za PASCH nchini Ujerumani na kupata uzoefu wa moja kwa moja.

Aidha, Goethe-Institut huongeza uelewa kuhusu fursa za kazi zinazotokana na ujuzi wa lugha ya Kijerumani. Wanafunzi wa shule za PASCH huhimizwa kuomba masomo ya chuo kikuu au mafunzo ya ufundi nchini Ujerumani.

Vijana huendelea kujihusisha na mpango huu hata baada ya kumaliza mtihani wao wa mwisho katika shule za PASCH. Kupitia mtandao wa wahitimu wa PASCH, Goethe-Institut huandaa mikutano ya wahitimu na kutoa nafasi za mawasiliano binafsi.

Takwimu na Maelezo

2008

ndio mwaka mpango ulipozinduliwa kwa mara ya kwanza na Goethe-Institut ikaanza kushirikiana na shule za mwanzo za PASCH.

125

ndizo nchi ambazo mtu angehitaji kusafiri ili kutembelea zaidi ya shule 700 za PASCH zinazoshirikiana na Goethe-Institut kwa sasa.

250.000

Wanafunzi wa PASCH wanaojifunza Kijerumani katika shule zinazoshirikiana na Goethe-Institut kwa sasa.

18.000

Wanafunzi duniani kote waliopewa ufadhili wa kuhudhuria moja ya kambi za vijana za PASCH tangu mwaka 2008.

PASCH-net

Tovuti ya www.pasch-net.de inatoa taarifa kuhusu taasisi washirika wa PASCH na shughuli zao duniani kote. Ramani shirikishi inaonyesha mtandao wa shule. Walimu na wanafunzi wao wanaweza kuperuzi matini ya kufundishia Kijerumani na kugundua shughuli mbalimbali za kushiriki.

Picha imechukuliwa kutoka kwa mtu aliyeshikilia kishikwambi. Skrini inaonyesha tovuti ya www.pasch-net.de ikiwa na michoro na picha zenye rangi mbalimbali. © PASCH-net © PASCH-net

Shule za PASCH nchini Tanzania

Kila shule ina upekee wake! Shule shiriki zinajitambulisha.

Mawasiliano

Washirika wa PASCH

Mpango wa PASCH unaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani na kutekelezwa kwa ushirikiano na Wakala Mkuu wa Shule za Nje (ZfA), Goethe-Institut, Shirika la Ujerumani la Ushirikishaji wa Kitaaluma (DAAD) na Idara ya Ushirikishaji wa Kielimu (PAD) ya Jopo la Mawaziri wa Elimu na Masuala ya Utamaduni wa Majimbo ya Ujerumani.

  • PASCH

Tufuatilie