Kozi ya mtandaoni kwa ajili ya kikundi

Jifunze Kijerumani kwa pamoja - mafunzo ya kusisimua kwa ushirikiano na kwa mtu mmoja mmoja

Wasiliana nasi
Illustration:  Erwachsene in einer Online Unterrichtssituation
  • jifunze kwa wakati wako
  • vipindi mubashara na mwalimu wako
  • majaribio shirikishi kupitia kikundi

Umakini na ufanisi

Unapenda kujifunza Kijerumani katika kikundi lakini huwezi  kufika katika kituo cha karibu cha Goethe-Institut? Una safari za kikazi na usingependelea kuhudhuria kozi mahali wala kwa muda mahsusi? Endapo ni hivyo, tuna ofa maalumu kwako! Kozi ya kikundi kwa njia ya mtandao ya "Deutsch Online" hukuwezesha kujifunza kwa wakati wako na ratiba yako na haikuhitaji kuwa mahali popote mahsusi. Badala ya kujifunza peke yako, unakuwa sehemu ya kikundi kidogo cha kati ya washiriki 10 hadi 18.

Kusoma, kuandika, kusikiliza, kuongea – Unaamua unavyotaka kujifunza kwa njia ya mtandao.  Unachagua kozi ya kikundi au kozi ya mtu mmoja mmoja na kama  unapenda   kujifunza kwa kujitegemea  au kuwa karibu na mwalimu.

  • Ngazi
    A1, A2, B1.1, B1.2

  • Inaanza
    wakati wowote

  • Mda
    wiki 10

  • Masaa ya kufundisha ndani ya wiki
    mara 2 kwa wiki

  • Upeo wa jumla
    vipindi 150 vya mafunzo

  • Washiriki
    idadi ya juu 18

  • Jukwaa la kujifunzia
    Kwa kipindi cha kozi

  • Bei
    TSH 700,000


Gruppe und Lerner an Laptop

Jinsi kozi inavyoendeshwa

Jukwaa la mafunzo
Kozi yako ya kikundi ya "Deutsch Online# ipo katika sura tofauti zinazoakisi mada na dhamira za kila siku, na pia itakufundisha matumizi yanayofaa ya msamiati na sarufi. Unajifunza kwa majaribio tofauti kupitia mtandao, kwa mfano video, picha, sauti, kusoma vifungu vya maneno na kujaza nafasi zilizoachwa wazi, kwa kujitegemea mwenyewe na kama kikundi. Tunakupatia maelezo unayoweza kupakua mtandaoni juu ya dhamira tofauti katika kozi ya Kijerumani.

Msaada kutoka kwa  mwalimu
Kazi ndefu za kuandikwa zinaweza kutumwa kwa mwalimu kupitia baruapepe, na zitarudishwa zikiwa na masahihisho na mrejesho wa kina. Endapo  una maswali yoyote,  unaweza kupiga soga na washiriki wengine  wa kikundi chako cha “Deutsch Online,” au baruapepe kwa mwalimu wako.

Mafunzo kwa njia ya mtandao kupitia vipindi mubashara
Kutana na mwalimu wako na washiriki wengine katika darasa lako la mtandaoni kupitia mfululizo wa vipindi. Lengo la vipindi hivi ni  kushughulikia mahsusi Kijerumani chako cha kuongea.


Maswali? Tupo hapa kusaidia: