Ulinzi wa Watoto

Schild mit Aufschrift "Kindergarten" © Goethe-Institut/ Gina Bolle

Iwapo unafanya kazi, unahitaji mja wa kumtunza mtoto wako. Maana ya malezi hayo ni,mja anamshughulikia mtoto wako. Kuna njia mbalimbali za malezi kupitia Kituo cha kulea watoto wachanga, vikundi vya michezo, nina/abu wa mchana, chekechea, kituo cha watoto wa shule au malezi ya mchana.

Audio-Player: Artikel anhören

Artikel anhören

Kinderbetreuung

Chekechea – kucheza pamoja, kujifunza pamoja

Nchini Ujerumani, watoto wengi huenda kwenye chekechea wakati wa mchana. Huko chekechea wanacheza na watoto wenzao na kupata wandani wapya. Mtoto wako anaweza pia kubaki chengoni kwako. Lakini chekechea zina faida nyingi. Mtoto wako anajifunza Kijerumani na mambo mengine huko.

Miji na halmashauri kulingana na ukubwa wake huwa na vituo vingi vya malezi ya watoto. Lakini pia kuna vituo vinavyoendeshwa na makanisa au taasisi nyingine kama Caritas. Kuna vituo binafsi vya malezi ya watoto na vile vilivyoanzishwa na wazazi wenyewe. Baadhi ya chekechea huwa ni za lugha mbili. Lugha mbili huzungumzwa huko, kwa mfano Kijerumani na Kihispania. Vilevile, kuna chekechea ambazo watoto hucheza nje siku nzima.

Gharama

Vituo vingi vya malezi ya watoto vinahitaji malipo. Vituo binafsi vya malezi ya watoto kwa kawaida hugharimu zaidi kuliko vile vya halmashauri. Gharama hutofautiana kati ya majimbo. Na sio kila mja ambaye hulipa kiasi sawa. Hii inategemea mambo mbalimbali.Je, kipato chako ni cha kiasi gani? Mtoto wako ana umri gani? Na anakaa kwa muda gani katika kituo cha malezi ya watoto? Katika baadhi ya majimbo na miji, malezi ya watoto huwa ni bure. Mara kwa mara huwa nafasi zote za malezi, wakati mwingine hupatikana chekechea pekee. Watoto wengi hupata chakula na vinywaji katika vituo vya malezi ya watoto. Kwa hivyo, unapaswa kulipia kiasi fulani kila mwezi. Ikiwa una kipato kidogo, kuna msaada unaopatikana. Kwa maelezo zaidi, unaweza kuuliza kituo cha Idara ya Ajira au ofisi ya ustawi wa jamii.

Usajili

Tangu mwaka 2013, watoto kuanzia miezi 12 wana haki ya kisheria ya kupata nafasi katika "Kita". Hii ina maana kuwa, kila mtoto kuanzia mwaka mmoja anaweza kuhudhuria kituo cha malezi ya watoto iwapo wazazi wake wanataka. Kwa bahati mbaya, mara nyingi haiwezekani. Kuna uhaba wa nafasi katika vituo vya "Kita" na uhaba wa walezi nchini Ujerumani. Unapaswa maana yake ni: Mahakama itaamua kama unastahili fidia. Kwa mfano, kwa sababu hutaweza kufanya kazi au utalazimika kufanya kazi kwa muda mchache kufwatia kukosa nafasi ya malezi. Au kwa sababu aina nyingine ya malezi ni ya gharama kubwa zaidi.

Watoto wadogo chini ya miaka 3

Wewe na mwenza wako mnafanya kazi na mna mtoto mdogo (kuanzia miezi michache hadi miaka 3)? Basi unaweza kumpeleka mtoto wako kwenye kituo cha kulelea watoto wachanga. Vituo vya kulelea watoto wachanga vina nafasi chache sana. Mara nyingi wazazi huwasajili watoto wao hata wakiwa bado wako katika ujauzito.

Mtoto wako anaweza pia kutunzwa na mlezi wa watoto wa mchana / nina au abu wa mchana. Malezi haya hufanyika chengoni mwa mlezi huyo. Wao huhudumia kundi dogo tu la watoto.

Ikiwa hauhitaji huduma ya malezi kwa kila siku, lakini wataka mtoto wako awe na mawasiliano na watoto wengine, kuna vikundi vya michezo. Wazazi na watoto wanaweza kuhudhuria vikundi hivi pamoja. Au watoto hutunzwa huko kwa masaa machache tu. Kuna pia matukio mengine ya wazazi na watoto kwa watoto wachanga Kwa mfano kupiga mbizi kwa watoto wachanga, kuimba pamoja au michezo ya harakati. Huko unaweza pia kukutana na wazazi wenzako.

Chekechea

Kuanzia miaka 3 hadi kusajiliwa shuleni, watoto huhudhuria chekechea. Huko wanaweza kucheza, kuimba, kuchora na kufanya kazi za mikono. Chekechea nyingi huwa na bustani kubwa. Katika majira ya kiangazi, waalimu wa chekechea mara nyingi huenda na watoto porini au katika matembezi mengine.

Si zaidi ya miaka 5, watoto wote wanapaswa kuhudhuria chekechea. Chekechea ni maandalizi muhimu kwa shule. Katika chekechea nyingi, kuna mipangilio ya kukuza mafunzo ya lugha. Hii huwasaidia watoto ambao bado hawawasiliani kutumia Kijerumani vizuri. Wakati mwingine hata watoto Wajerumani hupata shida na Kijerumani. Wakufunzi wa chekechea hucheza michezo ya lugha na watoto, huwasomea hadithi na kuwapa masimulizi.

Chekechea zinapatikana pia katika maeneo madogo. Msajili mtoto wako mapema katika chekechea. Hata hapa nafasi ni chache. Katika chekechea, mtoto wako atapata wandani, atawasiliana kutumia Kijerumani na kujifunza kuhusu nchi mpya kwa haraka.

Baadhi ya chekechea hufungwa saa za mchana (kuanzia saa 1 au 2 macheo hadi saa 6 au 7 mchana). Chekechea nyingine hufunguliwa siku nzima (kuanzia saa 1 au 2 macheo hadi saa 10 au 11 machweo).

Watoto wa shule

Watoto kuanzia miaka 6 au 7 ni sharti waende shule. Kuna sheria ya lazima kuhudhuria shule. Zaidi kuhusu hili utapata kwenye maandiko yetu ya taarifa “Mfumo wa Shule”. Iwapo unafanya kazi, mtoto wako anaweza kwenda shule ya siku nzima au baada ya shule aende kwenye kituo cha watoto wa shule au malezi ya mchana. Mara nyingi watoto hupata chakula cha mchana huko. Katika kituo cha watoto wa shule, mtoto wako anaweza kukaa hadi saa 10 au 11 machweo. Malezi ya mchana huwa ya muda mfupi zaidi.

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Tufuatilie