Die Flagge der Europäischen Union ist zu sehen. © Goethe-Institut

Muktasari

Umoja wa Ulaya ni shirikisho linalojumuisha nchi wanachama 27 kwa sasa ( kama ilivyo mwezi wa Januari 2020). Kuna lugha rasmi 24 ambapo nyaraka na taarifa zote hupatikana. Mfumo wa siasa wa Umoja wa Ulaya umejikita katika mikataba miwili ( Mkataba wa Umoja wa Ulaya  na Mkataba wa Utendaji wa Umoja wa Ulaya).  Zaidi ya yote Umoja wa Ulaya , unasimamiwa na taasisi tano: Baraza la Ulaya, Baraza  la Umoja wa Ulaya , Bunge la Ulaya, Tume ya Ulaya na mahakama ya Umoja wa Ulaya

Der Checkpoint Charly in Berlin zeigt die Geschichte Deutschlands. © Goethe-Institut

Historia

Ujerumani ni mojawapo  ya mataifa  sita yaliyoanzisha Umoja wa Ulaya wa leo baada ya vita vikuu vya pili vya dunia mnamo mwaka 1950. Mwanzoni , ilikuwa  hasa muungano wa kiuchumi uliowezesha biashara. Kwa hiyo, tangu mwaka 2002 kuna sarafu  moja ya Euro  kwa umoja wa nchi za ulaya 19. Kwa sasa, sera ya pamoja ipo pia katika mstari wa mbele:  kutoka mabadiliko ya tabia nchi ya uhifadhi wa mazingira na afya, na mahusiano ya nje na usalama, haki na uhamiaji .

Malengo na Thamani

Malengo ya Umoja wa Ulaya ni pamoja na kukuza amani na ustawi wa wananchi , pia uhuru na usalama na utawala wa sheria bila mipaka ya ndani. Uhusishwaji, uvumilivu, utawala wa sheria, umoja na kutokuwa na ubaguzi  ni maadili ambayo yanaunganisha nchi za wanachama wa Umoja wa Ulaya.Tangu kuanzishwa kwake hakukuwa na vita katika nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya. Usawa ni kigezo kingine cha Umoja wa Ulaya. Jambo ni kwamba wananchi wote wana haki sawa mbele ya sheria.  Usawa kati ya wanawake na wanaume ni sehemu ya sera zote za Umoja wa Ulaya na msingi wa ushirikiano wa Ulaya. Sera hizo , zinafanya kazi katika maeneo yote.

Kanuni ya kulipa kwa usawa kwa kazi sawa iliwekwa kwenye mkataba mwanzoni mwa mwaka 1957 lakini haijatekelezwa ipasavyo.

Auf einer Ampel zeigt das rote Licht ein gleichgeschlechtliches weibliches Paar und das grüne Licht ein gleichgeschlechtliches männlichs Paar. © Goethe-Institut

Bodi ya Usawa ya Umoja wa Ulaya

Lengo la  bodi ya usawa ni kusaidia wafanyakazi wa umoja wa ulaya kwa haki wanazonufaika nazo katika mfumo wa uhuru wa kusafiri au kutembea kwa wafanyakazi nchini Ujerumani. Inatoa ushauri binafsi wa kisheria/ au msaada mwingine  kupitia ushauri au ushauri wa rufaa pamoja na taarifa juu ya haki ya kusafiri au kutembea kwa wafanyakazi kwa uhuru. Taarifa hii  inapatikana kwa Kijerumani, Kiingereza, Kipolishi, Kihispania, Kifaransa, Kiromania, na Kibulgaria.

Tovuti husianishi

Video International Sign

Further questions? Write us via the contact form. We will forward your questions anonymously to the advisors of the youth migration services.

Contact form