Kuishi na Watoto

Kinderfahrrad und Schuhe vor einer Wohnungstüre © Goethe-Institut/ Gina Bolle

Akraba ni jambo la natija sana. Akraba hutoa upendo, msaada na mshikamano. Nchini Ujerumani kuna aina tofauti za akraba. Kila akraba ni ya kipekee.

Audio-Player: Artikel anhören

Artikel anhören

Leben mit Kindern

Maisha ya Familia

Katika akraba nyingi, wazazi wote wawili wanashiriki katika malezi ya watoto. Mara nyingi mzazi mmoja hufanya kazi kidogo ili aweze kutumia muda zaidi na watoto. Kwa kawaida huwa ni nina. Lakini kuna idadi inayoongezeka ya abu wanaoacha kazi kwa muda fulani ili kuwatunza watoto.

Wazazi wengine hutengana. Hata hivyo, wengi wao huendelea kuwatunza watoto kwa pamoja, hata kama hawaishi tena nyumba moja. Pia kuna akraba nyingi zinazoundwa na mzazi mmoja tu. Hawa huitwa wazazi walezi peke yao. Kuna akraba za upinde wa mvua ambapo watoto wana nina wawili au abu wawili. Kuna akraba za mseto, ambazo watoto kutoka akraba tofauti huishi pamoja. Pia kuna akraba za malezi, ambapo jamaa au walezi huwatunza watoto.

Ujauzito

Aushi ya pamoja na watoto huanza tangu kipindi cha ujauzito. Ikiwa una maswali kuhusu ujauzito, unaweza kwenda kwenye kituo cha ushauri wa ujauzito.

Wakati wa ujauzito, unapaswa kumtembelea daktari wa wanawake mara kwa mara. Daktari huyo atayajibu maswali yako na kufuatilia siha ya mtoto wako. Mkunga ana majukumu yanayolingana na ya daktari. Mkunga atakushauri na kukuauni wakati wa ujauzito na pia baada ya kujifungua. Mkunga pia huhudhuria wakati wa kujifungua. Daktari wako anaweza kukuauni kupata daktari wa wanawake na/au mkunga. Wanawake wengi pia hushiriki katika darasa la maandalizi ya kujifungua. Hapo utapewa ushauri mwingi kuhusu kujifungua. Pia utapata fursa ya kukutana na wanawake wengine wajawazito.

Likizo ya Uzazi, Likizo ya Wazazi na Msaada wa Wazazi

Ikiwa una kazi ya kudumu, unaweza kuchukua likizo ya Uzazi hata kabla ya kujifungua. Katika kipindi hiki hauhitaji kufanya kazi. Katika taaluma nyingi, likizo hii huanza majuma sita kabla ya kujifungua. Likizo ya Uzazi hudumu kwa angalau majuma 14. Unaweza kuongezewa. Katika kipindi hiki, mwajiri wako haruhusiwi kukusutisha kazi.

Baada ya likizo ya uzazi, unaweza kuchukua likizo ya mzazi: unabaki chengoni na kumtunza mtoto wako. Katika kipindi hiki hufanyi kazi. Likizo ya mzazi inaweza kudumu hadi miaka mitatu. Lakini unaweza pia kuchukua likizo ya mzazi ya mwaka mmoja au miwili tu. Sehemu ya likizo ya mzazi unaweza kuitumia hadi mtoto wako atakapofikisha miaka minane. Hili linawahusu wazazi wote wawili. Baadaye unaweza kurudi kwenye kazi yako.

Si rahisi kila mara kupatanisha kazi na akraba. Nchini Ujerumani kuna msaada wa wazazi. Lengo lake ni kusaidia akraba changa. Katika miezi kumi na mbili ya mwanzo wa likizo ya mzazi, unapata msaada wa wazazi. Ikiwa mwenzi wako pia anachukua likizo ya wazazi, basi kipindi hicho kinaongezeka hadi miezi kumi na minne. Kuna pia msaada wa wazazi Plus, ambao unaweza kupatikana hadi miezi 24. Kiasi cha msaada huo hutegemea mshahara wako wa mwisho baada ya makato. Lazima uombe msaada huo. Unastahili msaada huu hata kama huna kazi.

Pesa ya Watoto

Kuwatunza watoto kunahitaji gharama kubwa. Ndiyo maana akraba nchini Ujerumani hupokea hela kutoka kwa serikali. Hela hii ya watoto ina auni kuwahudumia watoto ili wawe na maisha mazuri na mustakabali bora. Sharti uombe hela hii katika Wakala wa Ajira ya Shirikisho. Unapokea hela ya watoto hadi angalau mtoto wako atakapofikisha miaka kumi na minane. Wale wanaopata mapato kidogo wanaweza pia kupata msaada wa ziada.

Vipimo vya Kinga

Siha ya watoto wako ni jambo la natija. Ndio maana nchini Ujerumani kuna vipimo vya mara kwa mara kwa watoto,vinavyofanywa na daktari wa watoto. Katika vipimo hivi vya kinga, daktari humdadisi mtoto wako kwa kina. Kwa njia hii matatizo na ndwele yanaweza kutambuliwa mapema. Daktari hudadisi mfano ,uzito na urefu wa mtoto wako. Anaangalia kama mtoto anakua vizuri. Kila uchunguzi hunakiliwa na daktari kwenye kijitabu maalum. Vipimo vya kinga hufanywa bure. Ni muhimu kuhakikisha huachi au kusahau vipimo hivi. Daktari pia ndiye anayepeana chanjo kwa mtoto wako.

Watoto Wenye Ulemavu

Je, una mtoto aliye na maumbile maalum au mwenye ugonjwa wa kudumu? Tafadhali soma taarifa katika maandishi yetu yenye kichwa “Ujumuishaji: Kuishi na Ulemavu.

Ulinzi wa Watoto

Nchini Ujerumani, kuna njia mbalimbali za kuwatunza watoto wako. Tafadhali soma maandiko yetu ya taarifa yaliyopewa jina "Ulinzi wa Watoto".

Burudani

Wakati wa mapumziko, unaweza kufanya mambo mengi pamoja na watoto wako: Kwa watoto wadogo kuna uwanja wa michezo nje. Watoto wakubwa wanaweza, kwa mfano, kujiunga na klabu ya michezo. Wakati wa kiangazi kuna mabwawa ya kupiga mbizi ya wazi, wakati wa baridi kuna mabwawa ya ndani ya kupiga mbizi. Wakati wa likizo za shule, miji huandaa shughuli maalum kwa watoto ambazo si za gharama kubwa. Taarifa zaidi unaweza kupata katika Mamlaka ya ustawi wa vijana na kwenye jumba la mji. Pia vilabu vingi vina shughuli za burudani maalum kwa watoto. Maelezo zaidi yapo katika maandiko yetu ya taarifa yaliyopewa jina "Burudani".

Watoto nchini Ujerumani mara nyingi hujumuika na wandani wao. Kwa mfano, hutembeleana chengoni na kucheza pamoja. Wakati mwingine watoto huwaalika watoto wenzao kuja kulala kwao chengoni. Watoto wengi husherehekea siku yao ya kuzaliwa kwa kuandaa sherehe. Kwa hiyo huwaalika watoto wengine. Sherehe hiyo mara nyingi hufanyika chengoni. Kuna michezo ya kufurahisha na keki. Pia kuna sherehe ambazo wazazi hufanya ziara pamoja na watoto.

Mizozo, Migogoro na Vurugu katika Familia

Aushi ya kiakraba si rahisi kila wakati. Na malezi ya watoto yanaweza kuwa ya kuchosha sana. Kipindi cha kubalehe, yaani wakati watoto wanapokua na kuwa waja wazima, pia si wakati rahisi. Maoni tofauti, kijicho au hali zisizotarajiwa za maisha pia zinaweza kusababisha mizozo na sintofahamu katika akraba. Vituo vya ushauri vinaweza kukuauni kutafuta ufumbuzi kwa pamoja.

Hali ni mbaya sana katika akraba yako? Kuna vurugu za kimwili au za kingono? Hata maneno yanaweza kuwa vurugu. Tafadhali tafuta msaada kwa haraka. Kuna namba za dharura na vituo vya ushauri. Usisite. Pia kuna msaada maalum kwa wanawake.

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Tufuatilie