Jibu la swali hili linategemea nchi unayotoka, sifa zako za kitaaluma, na umri wako.
Raia wa Umoja wa Ulaya (EU), Eneo la Kiuchumi la Ulaya (EWR), na Uswisi hawahitaji viza wala kibali cha kazi.
Raia wa Australia, Israeli, Japani, Kanada, Jamhuri ya Korea, Nyuzilandi, Ufalme wa Muungano wa Briteni Kuu na Ayalandi ya Kaskazini, pamoja na Marekani wanaruhusiwa kuingia Ujerumani bila viza.
Hata hivyo, bado wanapaswa kuomba kibali cha kazi, ambacho wanaweza kuwasilishia maombi yao moja kwa moja katika Mamlaka ya Uhamiaji nchini Ujerumani.
Iwapo unatoka nchi nyingine yoyote, utahitaji viza.
Unapaswa kuomba viza ya kufanya kazi nchini Ujerumani kupitia kwa Ubalozi wa Ujerumani (au Konseli ya Ujerumani) nchini kwako. Viza hii inahusisha pia kibali cha kazi; hivyo hautahitaji kuomba kibali hicho kwa utaratibu tofauti.
Kwa ajili ya kupata viza hii, pamoja na nyaraka nyingine, utahitaji:
- Pendekezo mahsusi la ajira au mkataba wa kazi
Sheria inasema wazi: ajira hiyo sharti iwe halali. Mamlaka ya Uhamiaji itawasiliana na Idara ya Ajira ambayo itadhibitisha kuwa masharti ya kazi na mshahara ni stahiki. Ikiwa masharti yanakubalika, wataidhinisha. Huna haja ya kuchukua hatua yoyote.
- Uthibitisho wa sifa zako za kitaaluma
Hili linahitajika iwapo unakusudia kufanya kazi katika taaluma zilizodhibitiwa kisheria, kama vile udaktari, ualimu wa chekechea, au kazi ya uuguzi.
Orodha ya taaluma hizi unaweza kupata hapa:
Kuna pia viza maalum kwa ajili ya mchakato wa uthibitisho wa sifa zako nchini Ujerumani:
Ikiwa wewe ni mfanyikazi wa kwa taaluma zisizodhibitiwa kisheria, masharti ya uthibitisho wa sifa mara nyingi huwa si magumu vile.
aelezo zaidi yapatikana: