Pasipoti na viza
Ili kuingia Ujerumani, unahitaji pasipoti halali au hati nyingine inayoithibitisha utambulisho wako. Pia utaihitaji pasipoti yako unapoenda kuhudumiwa ofisi mbali mbali za serikali. Raia ambao hawatoki Umoja wa Ulaya (EU) wanahitaji pia viza.