Masomo ya Chuo Kikuu

Hörsaal mit Dozent und Studierenden © Goethe-Institut

Ungependa kuhudhuria masoma ya chuo kikuu Ujerumani? Basi utahitaji cheti cha kuhitimu shule. Ukiwa wabaini cheti, unayo Haki ya Kujisajili kwenye Chuo Kikuu Ujerumani.

Visa, Shahada na Vyeti

Kama huna uraia wa Umoja wa Ulaya (EU) au Eneo la Uchumi la Ulaya (EWR), utahitaji pia visa. Visa hupatikana katika ubalozi wa Ujerumani au katika ofisi ya ubalozi mdogo nchini kwako. Pia, unatakiwa kuonyesha ushahidi wa fedha zitakazosimamia mahitaji yako ukiwa humo. Lazima udhibitishe kuwa una pesa za kutosha. Pia, unahitaji kuwa na bima ya afya.

Umeshamaliza masomo yako ya chuo kikuu? Wataalamu wenye ujuzi mkubwa wana nafasi nzuri Ujerumani. Hakikisha vyeti vyako kutoka nchi yako vimetafsiriwa na kuthibitishwa. Hii ni muhimu ili upate kibali cha kufanya kazi. Maelezo zaidi utayapata kwenye sehemu ya Utafutaji Ajira.

Chuo Kikuu na Kozi za Masomo

Nchini Ujerumani kuna vyuo vikuu mbalimbali vya serikali na vya kibinafsi. Iwapo unamiliki cheti cha kidato cha sita (Abitur) au cheti kingine kitakachokuruhusu kujisajili katika chuo kikuu, mtu anaweza kudurusu katika chuo kikuu (Uni) au chuo cha teknolojia (FH). Kwa cheti cha kidato cha sita cha teknolojia (Fachabitur), mtu anaweza kwenda chuo cha teknolojia na kudurusu masomo maalum tu katika chuo kikuu. Masomo katika chuo cha teknolojia huwa na mazoezi zaidi kuliko chuo kikuu.

Katika vyuo vikuu vya Ujerumani kawaida mtu anaweza kuhitimu shahada tatu:
  • Shahada ya kwanza (Bachelor)
  • Shahada ya uzamili (Master)
  • Mtihani wa kitaifa (Staatsexamen)
Nchini Ujerumani kuna kozi za masomo takriban 20,000. Mtu anaweza kusoma katika nyanja mbalimbali. Kuna pia kozi za kimataifa, kwa mfano kwa lugha ya Kiingereza.
Unatafuta kozi au chuo? Hifadhi data ya tovuti ya "Study in Germany" itakuauni kutafuta.

Vyuo vikuu vyote kwa kawaida huwa na Ofisi ya Maswala ya Kimataifa. Hapa wafanyakazi hupeana ushauri wao kwa wanagenzi na wadau wa kigeni kuhusu masomo nchini Ujerumani.

Pia kuna kozi nyingi zinazochanganya masomo ya chuo na kazi ya vitendo. Kozi ya mchanganyiko ni mchanganyiko wa masomo ya chuo na kazi ya vitendo katika kampuni. Wanagenzi hupata mshahara kutoka kwa kampuni.

Mahitaji

Kwa kawaida, ili kusoma shahada ya kwanza (Bachelor), unahitaji cheti cha kukamilisha shule. Hiki ni cheti cha kuhitimu elimu ya juu au cheti cha elimu ya juu ya ufundi (Fachhochschulreife). Shahada ya uzamili (Master) ni kiwango cha juu cha elimu ya chuo kikuu. Unaweza kudurusu shahada ya uzamili ikiwa tayari una shahada ya kwanza (Bachelor). Mtihani wa serikali (Staatsexamen) hufanywa tu kwenye kozi maalum kama Tiba, Sheria, Famasi, Kemia ya vyakula, na katika baadhi ya majimbo, Ualimu. Wanagenzi hufanya mtihani wa serikali.

Chuo kikuu ndicho kinachoamua kama una ujuzi wa msingi unaohitajika ili kuanza masomo ikiwa una vyeti vya elimu kutoka nchi za nje. Wasiliana na Ofisi ya Kimataifa ya Chuo Kikuu (pia inaitwa: International Office) ili upate maelezo zaidi. Kama bado hauna ufahamu ni chuo kipi ungependa kusoma, kituo cha huduma kinachoitwa “uni-assist” huchunguza kwa niaba ya vyuo vikuu vingi kama vyeti vyako vinakuruhusu kudurusu katika chuo kikuu cha Ujerumani. Taarifa zaidi zinapatikana kwenye www.uni-assist.de na www.anabin.de. Hata hivyo, uamuzi wa mwisho upo mikononi mwa chuo kikuu chenyewe.

Iwapo ungependa kudurusu chuo kikuu Ujerumani (iwe ni Uni au FH), sharti uwe unafahamu Kijerumani vizuri. Kama Kijerumani si lugha yako ya mama, unahitaji cheti kinachoonyesha unaelewa Kijerumani. Mara nyingi, wanataka ufaulu mtihani uitwao "Deutsche Sprachprüfung für den Hochschulzugang" (DSH) au TestDaF. Pia, kuna uwezekano kuwa Kuna mambo mengine wanayoyangalia, kama vile ufaulu wako shuleni. Vilevile, kuna baadhi ya kozi zina nafasi chache (Numerus clausus), hivyo ni vizuri kuulizia mapema kwenye chuo husika.

Kama cheti chako cha shule hakitoshi kujiunga na chuo kikuu Ujerumani, inabidi usome kwanza kwenye shule ya matayarisho iitwayo Studienkolleg. Huko, utafanya mtihani wa kujiunga. Ni sharti uwe unafahamu Kijerumani kiwango cha B1. Ukikamilisha Studienkolleg, unafanya mtihani mwingine uitwao "Feststellungsprüfung". Studienkolleg inachukua muda wa miezi sita (mihula miwili), lakini wakati mwingine ni fupi zaidi. Kudurusu huko ni bure, lakini unalipia ada ya muhula.
​​​​​​​
Kumbuka, vyuo vingi vina tarehe za mwisho za kuomba usajili. Kwa hiyo, kama unapanga kwenda kusomea Ujerumani, anza mchakato mapema.

Muendelezo na Muda wa Masomo

Mwaka wa masomo chuoni Ujerumani umegawanyika katika mihula miwili: muhula wa baridi na muhula wa joto. Kila muhula unachukua kama miezi sita. Katikati ya muhula kuna likizo ya kama miezi miwili na nusu. Likizo ya muhula wa joto huwa ndefu kidogo. Wakati wa likizo hakuna masomo, lakini wanagenzi hufanya mitihani, huandika kazi za likizo au kwenda kujifunza kazi (praktikum). Kozi nyingi huanza wakati wa muhula wa baridi.

Muda wa kusoma hutegemea kozi unayochukua. Kwa kawaida, kupata shahada ya kwanza Bachelor, huchukua mihula 6-8. Kwa kuendelea mihula 2-4 wagenzi hupata shahada ya Master. Mwisho mwa somo la shahada, mwanagenzi huaandika ripoti kubwa (Abschlussarbeit). Wakati mwingine sharti wanagenzi wafanye mtihani wa mazoezi. Kwa mitihani ya kitaifa (Staatsexamen) wanagenzi wanahitaji muda mrefu zaidi.

Masomo yako yatakuwa na vitu vingi. Kuna mihadhara na semina. Kwenye mihadhara, wanagenzi wengi hukaa kwenye ukumbi mkubwa na mkufunzi anafundisha. Wanagenzi husikiliza na kuandika. Semina zinakuwa na wanagenzi wachache na zinahusisha majadiliano zaidi.

Gharama

Gharama ya masomo inategemea jimbo la Ujerumani unalosoma. Kwa vyuo vya serikali, kusoma shahada ya kwanza (Bachelor) na shahada ya pili (Master) ni bure. Lakini, kila muhula unalipia huduma kama usimamizi, huduma za wanagenzi na tiketi ya usafiri (Semesterticket). Tiketi hii inakuwezesha kutumia usafiri wa umma bure. Kwa vyuo vya kibinafsi, ada ni kubwa zaidi.

Maswali ya Mara kwa Mara

Tufuatilie