Makazi

Mehrfamilienhaus © Goethe-Institut/ Simone Schirmer

Unatafuta nyumba nchini Ujerumani? Katika baadhi ya maeneo, ni rahisi sana kupata nyumba. Katika maeneo mengine, ni vigumu sana kupata nyumba. Anza mapema kutafuta na uwasiliana kwa upesi na mwenye nyumba, utakapoona tangazo linalokufaa.

Kutafuta nyumba

Kuna tovuti kadhaa za kutafuta nyumba mtandaoni, kwa mfano: Unaweza pia kukodisha chumba kwenye nyumba inayotumika na wenza wa kupanga (kifupi: WG). Katika WG, waja kadhaa huishi pamoja katika nyumba moja. Vyumba vya WG vinapatikana kupitia tovuti ya wg-gesucht.de. Pia kuna nyumba za upangaji wa muda. Nyumba hizi hukodishwa kwa kipindi cha muda maalum tu.

Katika magazeti mengi pia kuna matangazo ya nyumba, hasa siku za Ijumaa au Jumamosi. Matangazo ya nyumba hupatikana pia katika tovuti za magazeti. Unaweza pia kuulizia nyumba katika Idara ya Makazi ya jiji au halmashauri yako. Pia wakala wa nyumba anaweza kukuauni katika kutafuta.Ukipata nyumba kupitia kwao, utatakiwa ulipe ada. Kwa kawaida wakala hupokea kiasi cha kodi ya miezi 2 - 3 kama malipo ya huduma.

Kodi na Amana

Katika matangazo, mara nyingi huonyesha kiasi cha kodi unachopaswa kulipia kwa ajili ya hiyo nyumba. Lakini mara nyingi ni kodi bila gharama za huduma (kodi baridi). Unapaswa pia kulipa gharama za ziada kama vile maji, usafi wa ngazi na ubebaji wa taka. Joto na umeme vinaweza pia kujumuishwa katika gharama hizi za ziada, lakini hili hutofautiana. Muulize mwenye nyumba ni gharama zipi zinazojumuishwa na ni zipi unazopaswa kulipia kando.

Kodi baridi pamoja na gharama za huduma huitwa kodi ya jumla (kodi ya joto). Unapaswa kutuma kodi ya jumla mwanzoni mwa kila mwezi kwa mmiliki wa nyumba.

Kwa kawaida nyumba haziji na samani, lakini mara nyingi kuna meko. Vitu vilivyoachwa na mpangaji wa awali kwa mfano jokofu, kwa hali ya kawaida unapaswa kuvinunua. Hii inaitwa  (malipo ya fidia ya vitu vilivyoachwa).

Mara nyingi mwenye nyumba hutaka ulipe amana. Amana hii haiwezi kuzidi kodi baridi ya miezi 3. Utaregeshewa amana hiyo unapogura. Ukihitaji kufahamu kama kodi ya nyumba ni kubwa kupita kiasi, unaweza kuangalia kwenye “Mietspiegel” yaani orodha ya viwango vya kodi. Hapo utapata wastani wa viwango vya kodi kwa kila jiji. Kwa maelezo zaidi ,tafuta kwenye mtandao kwa kuandika neno "Mietspiegel "pamoja na jina la jiji lako.

Mwanzoni mwa mwaka huwa haijulikani kiasi cha maji, umeme au gesi utakayotumia. Hivyo hulipia kiasi cha makadirio kila mwezi. Mwishoni mwa mwaka utarejeshewa hela au utatakiwa kuongeza kiasi fulani.

Mkataba wa upangaji

Maelezo yote kuhusu kodi na amana huandikwa kwenye mkataba wa upangaji. Pia unaelezwa kuwa unapaswa kuikarabati nyumba kabla ya kuondoka. Mara nyingi utatakiwa kutia sahihi kwenye fomu ya makabidhiano unapoingia kwenye nyumba hiyo. Fomu hiyo itakuelezea kuwa, iwapo kuna kitu kilichoharibika. Hii inathibitisha kwake mwenye nyumba kuwa hukukiharibu wewe.

Soma kwa makini mkataba wa upangaji na fomu ya makabidhiano kabla ya kuitia sahihi.

Ukitaka kugura, Kwa kawaida unatakiwa kupeana ilani ya miezi 3 kabla. Hii inaitwa kipindi cha ilani ya kusitisha upangaji. Kumbuka kipindi hiki ili usilipie kodi mara mbili. Ili kupeana ilani, andika barua kwa mwenye nyumba mwishoni mwa mwezi.

Kanuni za nyumba

Ikiwa hutaki mizozo na majirani zako, basi fuata kanuni za upangaji unakoishi. Kwa kawaida kuna muda wa utulivu kuanzia saa nne usiku hadi saa moja macheo, na muda wa mapumziko ya mchana kuanzia saa saba hadi saa tisa mchana. Katika kipindi hiki hakupaswi kuwa na kelele nyingi. Jumapili na siku za sikukuu, kuna utulivu siku nzima.

Kuna mapipa tofauti ya takataka kwa ajili ya karatasi na kasha, masazoi ya matunda na mboga, na takataka nyinginezo. Mara nyingi mapipa haya huwa mbele ya nyumba. Hapo ndipo unapoweza kutupa taka. Chupa au vifaa vya umeme vinapaswa kupelekwa kwenye vituo maalum vya ukusanyaji au kwenye kontena. Plastiki, makopo na taka za vifungashio hutupwa kwa kutumia mfuko wa manjano au pipa la manjano. Katika miji, mara nyingi hutakiwa kupeleka plastiki na vifungashio kwenye pipa maalum la kuchakata taka lililo karibu. Tafuta taarifa zaidi kutoka kwa jiji au halmashauri yako.

Kanuni nyingine zote utazipata katika kanuni za nyumba yako. Kwa mfano: Je, unaruhusiwa kuwa na jibwa au paka ndani ya nyumba? Au: Je, unapaswa kusafisha baraza au njia ya mbele ya nyumba?

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Tufuatilie