Upatikanaji wa haraka :

Nenda moja kwa moja kwenye maudhui (Alt 1) Nenda moja kwa moja kwenye ngazi ya kwanza ya urambazaji (Alt 2)

Kozi kwa makampuni

Eine Gruppe junger Geschäftsleute in einem Sitzungsraum; eine junge Frau reicht einem Mann die Hand.
  • Kwa njia ya mtandao au ana kwa ana
  • yenye kuzingatia mahitaji yako
  • ratiba inayobadilika kirahisi

Wafanyakazi wako ni mtaji wako? Je, kampuni yako ingeongeza ushindani na kupata faida zaidi endapo wafanyakazi wako wangekuwa na stadi za lugha ya Kijerumani? Huu ni wakati  kuwekeza katika mafunzo yao.

Sisi ni vinara wa lugha ya Kijerumani duniani. Kampuni yako inaweza kutegemea  ujuzi wetu na kigezo kwamba tumekuwepo Tanzania kwa zaidi ya miaka 20. Sisi kutoka Goethe-Institut Dar es Salaam  tutakusaidia kufikia malengo yako kupitia kozi zetu za lugha na mafunzo yenye kujali mahitaji ya mteja na tamaduni tofauti.

Huduma zetu

Firmenkurse Foto: Getty Images

Kozi ya kikundi ofisini kwako

Wape wafanyakazi wako fursa ya  kuendeleza stadi za lugha ya Kijerumani. Mbinu zetu za kisasa za ufundishaji na msaada kwa mtu mmoja mmoja hufanya mafunzo kuwa raha, washiriki hubaki na motisha kubwa huku wakipiga hatua kwa haraka.
Drei Frauen vor Laptop © Getty Images

Kozi kwa njia ya mtandao kwa makampuni

Kozi Zetu za Kikundi kwa Njia ya Mtandao hutumia mazingira halisi ya maisha  kutoa muktadha wenye uhalisia wa kujifunza Kijerumani. 
Je, unapenda kufahamu stadi za lugha za waombaji wa kazi au wafanyakazi wako? Fahamu bayana kwa dakika 60 tu  kupitia mtihani wetu wa kujipima kwa lengo hili:​​​​​​​
Goethe-Test PRO: Deutsch für den Beruf

Tutafurahi kukushauri  na pamoja kufanya uchaguzi unaofaa wa kozi kwa kampuni yako na wafanyakazi wako.
Juu