Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tutakujulisha hapa juu ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu mitihani ya Goethe-Institut.

Endapo una maswali zaidi kuhusu vyeti vya Goethe hatua ya A1 hadi C2, tafadhadi fanya mpango wa kupewa taarifa bila malipo yoyote kutoka moja ya maeneo yetu ya mtihani (Ofisi za Goethe-Institut, Vituo vya Goethe au wakala wa mitihani ya Goethe).

Mitihani ya Goethe-Institut ipo kwa ajili ya mtu yeyote apendaye, bila ya kujali uraia wa mtahiniwa. Imetungwa mahsusi kuonesha kiwango cha ujuzi wa Kijerumani kama lugha ya pili/au lugha ya kigeni.
Tunapendekeza umri wa chini wa watahiniwa wa mitihani
Unaweza kutoka nje ya chumba cha mtihani kwa muda unaoeleweka (mfano kwenda msalani). Ruhusa ya kutoka nje itaonekana kwenye ripoti ya msimamizi wa mtihani
Mitihani wa Goethe-Zertifikats kuanzia ngazi ya A1 hadi C2 inakidhi vigezo vya Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR). Angalia daraja ambamo umewekwa:
Upangaji wa madaraja ya hatua za mitihani ya Goethe-Institut na kozi za lugha
Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (KIJERUMANI)
Barua yenye maelezo juu ushiriki katika kozi ya lugha, tathmini ya majaribio, mtihani, nk. Havitoshi.

Ni cheti cha mtihani kinachoonesha umefaulu mtihani wa Goethe (Hatua ya A1 hadi C2, Kleines or Großes Sprachdiplom) ndicho pekee kinachotambulika kama ushahidi wa kiwango cha ujuzi wa lugha ya Kijerumani kama lugha ya pili.
Goethe-Zertifikat C2: Großes Deutsches Sprachdiplom, Zentrale Oberstufenprüfung (ZOP), Kleines Deutsches Sprachdiplom (KDS) na Großes Deutsches Sprachdiplom (GDS) ndiyo mitihani inayotambulika kwa mtu kujiunga na chuo/chuo kikuu nchini ujerumani, na kufanya mitihani hiyo hakuna haja tena ya kufanya mtihani wa TestDaF au mwingine kama huo.

Ili kufahamu zaidi juu ya mahitaji ya lugha kwa chuo kikuu husika na/au kozi au fani ya masomo nchini Ujerumani, omba taarifa moja kwa moja kutoka chuo kikuu, au tembelea www.sprachnachweis.de.
Tahajia inayotumika kwa upande wa mitihani yote ya kuandika ya Goethe ilitolewa Agosti 2006. Msingi wake unatokana na „DUDEN. Die deutsche Rechtschreibung“ (kulingana na toleo la 24, 2006) na „WAHRIG. Die deutsche Rechtschreibung“ ( toleo la 2006).

Kanuni zinazotumika sasa zinaweza kupatikana kutoka:
Duden. Die deutsche Rechtschreibung
Der Duden Produktkatalog
Bertelsmann WAHRIG. Verlagsprogramm
Institut für Deutsche Sprache (IDS)
DUDEN. Sprachberatung
Kujifunza ni mchakato wa mtu binafsi. Muda utakaochukua kuweza kufikia hatua fulani ya lugha  hutegemea mambo kadhaa ya binafsi: kujituma kwako, muda unaowekeza, na jinsi unavyotumia matini ya ziada ya mazoezi.

Endapo umewahi kujifunza lugha moja au zaidi hapo awali, unaweza kujifunza Kijerumani kwa haraka. Pia kuna tofauti kubwa kama unashiriki kozi ukiwa nchini kwako au ukiwa Ujerumani, ambapo utakutana na lugha ya Kijerumani nje ya darasa.

Pia jambo jingine ni mkazo katika mafunzo (mfano, mafunzo ya kina dhidi ya mafunzo ya jioni). Tafadhali wasiliana na kituo cha mtihani kilicho karibu ili upate maelekezo binafsi.
Kwa mtihani wa kila hatua utapata "taarifa na matini ya mazoezi" kwa kupakua mtandaoni
  • bila malipo
  • kwa kuagiza zaidi
Unaweza pia kupata matini ya mazoezi kutoka idara ya lugha ya Goethe-Institut iliyo karibu nawe.
Baadhi ya mitihani hutoa matini ya kujifunza kwa masafa na kozi kwa njia ya mtandao.
Kujifunza Kijerumani kwa njia ya masafa
Unaweza kurudia kufanya mtihani wote mara nyingi kadri unavyohitaji. Maelezo juu ya kurudia mtihani au sehemu ya mtihani yanapatikana chini ya masharti na vigezo vya kufanya mtihani
Goethe-Zertifikat A1: Fit in Deutsch 1
Mtahiniwa atachukuliwa kuwa amefaulu mtihani endapo atafikisha walau alama 30  (sawa na 50% ya alama ya juu kabisa) na endapo amejibu maswali kutoka seksheni zote za mtihani.

Goethe-Zertifikat A1: Start Deutsch 1
Mtahiniwa atachukuliwa kuwa amefaulu mtihani endapo atafikisha walau alama 60  (sawa na 60% ya alama ya juu kabisa) na endapo amejibu maswali kutoka seksheni zote za mtihani.

Goethe-Zertifikat A2
Goethe-Zertifikat A2: Fit in Deutsch
Goethe-Zertifikat C1
Mtahiniwa atachukuliwa kuwa amefaulu mtihani endapo atafikisha walau alama 60  (sawa na 60% ya alama ya juu kabisa) na endapo amejibu maswali kutoka seksheni zote za mtihani. Katika alama hizi, anatakiwa apate walau alama 45 kwenye mtihani wa kuandika na walau alama 15 kwenye mtihani wa kuongea. Vinginevyo, atachukuliwa kuwa amefeli mtihani wote.

Goethe-Zertifikat B1
Goethe-Zertifikat B2 (modular)
Goethe-Zertifikat C2: Großes Deutsches Sprachdiplom
Mtahiniwa atachukuliwa kuwa amefaulu moduli endapo atafikisha walau alama 60 au 60%.

Unaweza kupata taarifa zaidi juu ya vyeti vya Goethe kwa kubofya kitufe chenye jina la mtihani.

 
Vyeti vya Goethe-Zertifikats hatua ya A1 hadi C2 havina tarehe ya mwisho ya kuvitumia.

Hata hivyo taasisi na waajiri wengi hutarajia cheti kiwe kimetolewa ndani ya miaka miwili iliyopita.

Vyeti vya Zentrale Oberstufenprüfung (ZOP), das Kleine Deutsche Sprachdiplom (KDS) na das Große Deutsche Sprachdiplom (GDS) vitakuwa halali baada ya kuanza kwa Goethe-Zertifikat C2: Großes Deutsches Sprachdiplom na pamoja na mabadiliko ya matangazo ya mtihani wa hatua ya C2 utakaoanza 01.01.2012.
Hakuna nakala itakayotolewa

Endapo mtihani ulifanyika ndani ya miaka kumi iliyopita, kituo ulichofanyia mtihani kitakupatia hati mbadala kwa ada kidogo.
Kwa suala la jina kubadilika (mfano kupitia ndoa, kuasili, talaka, nk.), hakuna cheti kipya wala hali mbadala vitakavyotolewa

Mabadiliko ya jina yanaweza kuthibitishwa kwa nyaraka rasmi kutoka mamlaka husika (msajili wa cheti za kuzaliwa, leseni za ndoa, nk.) au nakala iliyothibitishwa rasmi na mamlaka hizo hapo juu.

Jina/ herufi za jina sharti ziingizwe kwenye kitambulisho cha picha wakati wa kujiandikisha kwenye kituo cha mtihani. Cheti cha mtihani kitatolewa kulingana na taarifa binafsi za awali zilizopo katika kumbukumbu.
Unaweza kutengeneza nakala iliyothibitishwa rasmi ya cheti chako - kwa mfano, kwa malengo ya kusoma nchini Ujerumani - kupitia kwa msajili wa viapo (mahakama, ofisi ya serikali, shule, benki, nk.). Mara nyngi waajiri hupendelea nakala iliyothibitishwa rasmi kupitia ofisi ya wakili.
Ufasiri rasmi unaweza kuandaliwa na mfasiri anayetambuliwa na serikali au ofisi ya ufasiri.
Ili uweze kufanya mtihani, hakuna haja ya kuthibitisha kuwa uliwahi kuhudhuria mafunzo ya lugha, kozi ya maandalizi au kupata cheti cha hatua ya chini.

Hata hivyo tunahimiza ushiriki katika kozi ya maandalizi kwenye kituo cha mtihani. Katika kozi hiyo utajifunza ujuzi wa lugha na mbinu mahsusi za stadi za lugha zitakazokusaidia kufaulu mtihani.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na kituo cha mtihani kilicho karibu ili upate maelekezo binafsi.
If you took your exam at a Goethe-Institut and have not received any other information, you can view your exam results at Mein Goethe.de.


Help with registration on My Goethe.de:
© Goethe-Institut


Help with retrieving exam results:
© Goethe-Institut

If you have any questions, please contact your Goethe-Institut directly.

If you took your exam with an examination partner working with the Goethe-Institut, please contact your examination centre directly.