Kuwasiliana na dunia. Kwa hali anuwai, maelewano na kuaminiana.
Tunaleta watu pamoja duniani kote. Kama taasisi ya utamaduni ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani, tunachochea ufungamano katika utamaduni, elimu na harakati za kijamii katika muktadha wa kimataifa, na kusaidia katika ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya Kijerumani. Pamoja na washirika wetu, tunatazama fursa na changamoto zinazoikabili dunia, kuleta pamoja fikra tofauti katika majadiliano yenye msingi wa kuaminiana. Tunachukulia uwezo wa kusikiliza na kutafakari kama msingi maelewano. Tunafuata kanuni za uwazi, hali ya kuwa anuwai na uendelevu. Kanuni hizi hutoa taswira ya huduma na mtindo wetu wa kufanya kazi.
Taasisi ya Goethe-Institution inawaalika wataalam na wabunifu ulimwenguni kubadilishana mawazo juu ya uhusiano wa nguvu ya wakoloni, matokeo yao na, zaidi ya yote, jinsi ya kuwasambaratisha: katika hotuba, mahojiano, nakala za maoni na miradi ya sanaa. Kwa ulimwengu usiotumikishwa na usio na ubaguzi.