Kazi

Goethe-Institut career Foto: Goethe-Institut/Loredana LaRocca

Tunasifika kwa kujumuisha watu wote bila ubaguzi, udadisi na uwazi. Goethe-Institut ni taasisi ya utamaduni ya Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani inayofanya kazi duniani kote. Tunasimamia mafunzo ya Kijerumani nchi za nje na kuhimiza kushirikishana utamaduni duniani. Tunaonesha taswira halisi ya kila siku ya Ujerumani na kutoa habari kuhusu hali ya utamaduni, jamii na siasa ya taifa letu.