Upatikanaji wa haraka :

Nenda moja kwa moja kwenye maudhui (Alt 1) Nenda moja kwa moja kwenye ngazi ya pili ya urambazaji (Alt 3)Nenda moja kwa moja kwenye ngazi ya kwanza ya urambazaji (Alt 2)
Mann am Laptop© Getty Images

#bakinyumbani
Jifunze Kijerumani Mtandaoni

Jifunze kijerumani – mtandaoni. Nenda na wakati na ujifunze kidijitali. Wakati wowote na mahali popote! Jiunge nasi ujipatie uzoefu wa kujifunza kwa mtindo wa kushirikishana na utakaokupa raha kutoka kwa wataalamu waandamizi katika nyanja za mafunzo ya lugha kwa mbinu ya kidijitali. Fanya majadiliano mubashara kwa njia ya ujumbe wa maandishi baina yako na mkufunzi wetu utumie majukwa yetu ya mafunzo kufanya mazoezi. Karibu ujifunze Kijerumani pamoja nasi. Mtandaoni.

Tarehe na ada
Lernplattform

Kujifunza mwenyewe

Jifunze mwenyewe nyenzo za kujifunzia zilizobuniwa kwa uhodari na rahisi kutumika kutoka kwenye jukwaa la mafunzo. Kwa namna unayopenda unaweza kujipangia majaribio yako moja kwa moja mtandaoni na kupokea mrejesho wa papo kwa hapo. Kwa viwango vyote vya uwezo na mahitaji ya lugha

Live-Sitzungen

Vipindi Mubashara

Jifunze kupitia vipindi mubashara kwa njia ya mtandao utakapomkuta mwalimu na wanafunzi wenzako. Kwa ajili hii tunatumia programu ya Adobe Connect, inayokupa uwezo wa kujifunza kana kwamba upo kwenye darasa la kawaida! Utapokea mrejesho wa mwalimu wako katika mazoezi ya kuongea na kuandika

Support

Usimamizi

Mwalimu wako atakupatia maelekezo jinsi ya kutumia nyenzo za mawasiliano pamoja na jukwaa la mafunzo. Wakati wa kozi, utapokea mrejesho wa mara kwa mara kwa kupitia nyenzo na jukwaa hilo.


Kozi ya mtandaoni kwa ajili ya kikundi

Kozi yetu makini inayotoa uhuru wa nyongeza

Kozi yetu ya mtandaoni kwa ajili kikundi ni mahsusi kwa wale wanaotaka uhuru wa kujifunza Kijerumani kwa jinsi wanavyopenda wakati huohuo wakiwa na hisia ya kujifunza katika kikundi. Stadi zote nne za umahiri katika lugha (kusoma, kuandika, kuongea, kusikiliza) hufundishwa. Kozi hufanyika kwenye jukwaa la mafunzo la Goethe-Institut na katika darasa la mtandaoni. TZS 550,000 ​– Shika Nafasi Sasa

  Kozi ya Mtandaoni kwa Kikundi
Hatua A1, A2 au B1
Tarehe ya Kuanza na Kumaliza 07.09.2020 – 18.12.2020
Muda wa Kozi Wiki 16
Uhuru katika Kujifunza Jumla ya vipindi mubashara 2-3 kwa wiki, kwa mkupuo au kwa awamu kama upendavyo
Kujifunza Kupokea mafunzo, hamasa na msaada katika kikundi.
Mrejesho Mrejesho wa kawaida, kwa mtu mmoja mmoja.

Mwalimu atatoa maudhui ya ziada endapo yanahitajika.
Idadi ya Washiriki wasizidi 18
Mahali na muundo katika hali tuliyonayo Kozi hii inafanyika kwa njia ya intaneti tu kupitia jukwaa la mafunzo na darasa la mtandaoni la Goethe-Institut kwa kutumia programu ya Adobe Connect
Ada TZS 500,000
TZS 550,000 ​– Shika Nafasi Sasa

Kozi ya mtandaoni - kwa mtu mmoja mmoja

Kwa mahitaji ya kila mtu mmoja mmoja

Kwa kupitia Kozi ya Mtandaoni ya Kijerumani kwa mtu mmoja mmoja unaweza kujifunza kusoma, kuandika na kuongea kwa uhuru kabisa. Unaweza kujipangia mwenyewe utasoma kwa mwendo gani. Mkufunzi wako atakupatia mrejesho wako pekee kwa muda wote wa kozi. Kozi itaendeshwa kupitia jukwaa la Goethe-Institut mtandaoni. Pia utakuwa na vipindi viwili au vitatu mubashara baina yako na mwalimu wako kupitia darasa la mtandaoni, kulingana na kiwango cha umahiri wa lugha.

Taarifa zaidi

  Kozi ya Mtandaoni kwa Mwanafunzi mmoja
Hatua A1, A2, B1.1 au B1.2
Tarehe ya Kuanza na Kumaliza Muda wowote
Muda wa Kozi Hadi kufikia miezi 6
Uhuru katika Kujifunza Jumla ya vipindi mubashara 2-3 kwa week, kutegemeana na umahiri wako wa lugha. Unaamua mwenyewe kuhusu wakati na spidi ya kozi kadri unavyopenda
Kujifunza Kupokea mafunzo binafsi ya stadi zote za lugha kwa spidi yako
Mrejesho Mrejesho wa kawaida, kwa mtu mmoja mmoja.

Mwalimu atatoa maudhui ya ziada endapo yanahitajika.
Washiriki Ni wewe tu na mwalimu wako.
Mahali na muundo katika hali tuliyonayo Kozi hii inafanyika kwa njia ya intaneti tu kupitia jukwaa la mafunzo na darasa la mtandaoni la Goethe-Institut kwa kutumia programu ya Adobe Connect
Ada TZS 30,000 kwa kipindi kimoja
B1.1 + B1.2 kila moja inahitaji vipindi 60
Taarifa zaidi
Ni wewe tu na mwalimu wako.

Jaribu kozi zetu

Unaweza kujiuliza akilini mwako ni jinsi gani Kozi za Mtandaoni tunazotoa hufanya kazi? Tunatoa wigo wa kozi mbalimbali kwa kwa Wanafunzi Waanzao na Waliopiga Hatua katika mfumo wa toleo la majaribio.

A young man and a young woman greet each other. © puhhha/Shutterstock

Trail Chapter A1 – First Steps
Hallo, wie geht's?

Here you will learn  the times of the day, how to greet someone in German and how to introduce yourself.

Fruits, vegetables and berries © marilyn barbone / Adobe Stock

Trial Chapter A1
Eating and drinking

Here you will learn words about food and drink and how to express quantities when out shopping.

A waiter directs a young couple to their table in the restaurant.

Trail Chapter A2
At the restaurant

Here you will learn how to order in the restaurant, how to ask for the bill and how to tip.


Maswali ya mara kwa mara

  • Programu inayoendesha mfumo wa kompyuta yako: kama vile Windows, MacOS
  • Programu ya kuvinjari mtandaoni: kama vile Google Chrome ®, Microsoft Edge ®, Mozilla Firefox ®, Apple Safari ® katika toleo la kisasa
  • Kipeo kinachoitwa Bandwidth: kinachofikia 512 kbps
  • Kifaa chako (kompyuta au simu) kiwe uunganishwa katika mtandao wa intaneti na barua pepe, pamoja na programu ya Adobe Connect ® kwa ajili ya kushiriki vipindi mubashara vya mtandao, pia uwe na spika ndogo za kupachika au kuweka sikioni
Tunapokuwa kwenye nyakati ngumu sana au kupitia mabadiliko yasiyo ya kawaida katika hali ya mambo iliyozoeleka na ambayo ipo nje ya uwezo wa Goethe-Institut (kama vile Machafuko, mithili ya vita au vitendo vya kigaidi, majanga ya asili, magonjwa ya mlipuko na mambo yanayofanana na hayo), tuna haki ya kutoa mbadala wa huduma (kama vile mabadiliko katika muda na/au mahali). Katika hali kama hiyo tutatoa tangazo juu ya huduma mbadala ndani ya muda unaofaa litakaloambatana na ombi juu ya ridhaa yako ya kutibitisha endapo unakubaliana na huduma hiyo mbadala iliyopendekezwa au endapo ungependa kujiondoa kutoka kwenye mkataba.
Endapo utachagua kujiondoa kutoka kwenye mkataba, tutarejeshea ada yote iliyolipwa (endapo sehemu ya huduma zitolewazo itakuwa tayari imetumika, ni sehemu ya ada ambayo itarudishwa).
Kwa sasa hatutoi kozi zozote kwa watoto au vijana.
Unaweza kupata tarehe sahihi za kozi za madarasani kwenye ukurasa wa Tarehe na ada na tarehe za mitihani kwenye ukurasa wa Tarehe na Kujiandikisha

 
Endapo tutaingia kwenye nyakati ngumu sana au kupitia mabadiliko yasiyo ya kawaida katika hali ya mambo iliyozoeleka (kama vile Machafuko, mfano wa vita au vitendo vya kigaidi, majanga ya asili, magonjwa ya mlipuko na mambo yanayofanana na hayo) ambayo yatakuwa nje ya uwezo wa Goethe-Institut, tuna haki ya kutoa mbadala wa huduma (kama vile mabadiliko katika muda na/au mahali). Katika hali kama hiyo tutatoa tangazo juu ya huduma mbadala ndani ya muda unaofaa litakaloambatana na ombi juu ya ridhaa yako ya kutibitisha endapo unakubaliana na huduma hiyo mbadala iliyopendekezwa au endapo ungependa kujiondoa kutoka kwenye mkataba.
Endapo utachagua kujiondoa kutoka kwenye mkataba, tutarejeshea ada yote iliyolipwa (endapo sehemu ya huduma zitolewazo itakuwa tayari imetumika, ni sehemu ya ada ambayo itarudishwa).
Endapo una maswali ya ziada, tafadhali tuma kupitia anuani: joseph.malumbo@goethe.de

Mawasiliano

You have more questions about our courses? Write to us! We are happy to help.

Joseph Malumbo
Head of Language Courses
Tel. +255 22 213 4800
joseph.malumbo@goethe.de


Kujifunza, kusoma kufanya utafiti mtandaoni

Jibweteke - Jifunze kijerumani nyumbani

Kupitia dondoo na majaribio yetu kwa njia ya kidijitali unaweza kujifunza Kijerumani kutokea nyumbani ukiwa umejitenga na wengine.

#onlinestattpräsenz © Getty Images

Maandalizi ya mtihani mtandaoni

Furahia matumizi bila malipo ya nyenzo zetu za majaribio kujifunza kusikiliza, kusoma, kuandika na kuongea katika maandalizi yako ya mitihani ya Goethe-Zertifikat.
 

Deutsch für dich Foto: Shutterstock.com, Rawpixel.com

goethe.de/deutschfuerdich
Deutsch für dich

Katika jumuiya ya “Deutsch für dich” utapata majaribio mengi sana ya kukusaidia kujifunza Kijerumani bila malipo yoyote, na unaweza kushirikishana uzoefu na wanachama wengine.

Juu