Goethe-Zertifikat A1: Fit in Deutsch 1

Goethe-Zertifikat A1: Fit in Deutsch 1 Foto: Getty Images/Echo

Unafaa endapo unataka

  • kufanya mtihani wa Kijerumani kwa watoto na vijana kati ya miaka 10 hadi 16
  • kuonesha kuwa una kiwango cha msingi cha uelewa wa Kijerumani 
  • kuthibitisha kuwa umefaulu kufika hatua A1
  • kupata cheti rasmi kinachotambulika kimataifa

Goethe-Zertifikat A1: Fit in Deutsch 1 ni mtihani wa Kijerumani kwa watoto na vijana wenye umri kati ya miaka 10 hadi 16. Unathibitisha kuwa mtahiniwa ameweza kupata maarifa ya msingi ya stadi wa lugha kulingana na hatua ya kwanza (A1) kwenye ngazi yenye hatua sita za umahiri na umezingatia Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR).

Kufaulu mtihani inamaanisha kuwa unaweza …

  • kuuliza na kujibu maswali mepesi pamoja na kuomba msaada au kitu fulani na kujibu unapoombwa,
  • kuandika taarifa zako binafsi na za wengine kwa kutumia sentensi nyepesi
  • kuelewa mazungumzo na maelezo juu ya mada zilizozoeleka

Maandalizi

Matini ya mazoezi

Mitihani ya mfano na matini ya kufanyia majaribio ambazo ni rahisi kutumia kukusaidia mtandaoni vinapatikana hapa

Maelezo zaidi

Mahitaji, yaliyomo katika mtihani na maelezo zaidi juu ya mtihani wa Goethe-Zertifikat A1: Fit in Deutsch 1 yanapatikana hapa: