Mtihani wa papo hapo wa kujipima kwa njia ya mtandao
Mtihani huu wa kujipima umesanifiwa ili kupima stadi zako za lugha ya Kijerumani, uwe ni mzoefu au ndio kwanza unaanza kujifunza lugha. Utajaribiwa katika usomaji wako kwa ajili ya kupima ufahamu na maarifa katika sarufi na msamiati.
Endapo una shauku ya kufanya kozi ya Kijerumani kutoka Goethe-Institut, tafadhali weka miadi ya kufanya mtihani wa kujipima kwa njia ya mtandao.
-
makadirio ya kipimo cha stadi zako za lugha ya Kijerumani
-
kipindi cha dakika 15-20
-
bila malipo