Upatikanaji wa haraka :

Nenda moja kwa moja kwenye maudhui (Alt 1) Nenda moja kwa moja kwenye ngazi ya kwanza ya urambazaji (Alt 2)

Mawasiliano na Kujiunga

contact and information Foto: Getty Images

​#bakinyumbani

Endelea kujifunza Kijerumani – mtandaoni. Katika kulinda afya yako, kwa sasa tunatoa kozi zote za lugha ya Kijerumani katika mfumo wa kupitia mtandaoni.

Masomo yetu mtandaoni

Je, umevutiwa na moja ya kozi zetu au unahitaji taarifa zaidi? Unaweza kutembelea ofisi yetu ya kozi za lugha kwa ushauri binafsi

Usisite kuwasiliana nasi endapo una maswali juu ya kujifunza Kijerumani kutoka Goethe-Institut Tanzania.

Tembelea Ofisi ya Kozi za Lugha:

Jumatatu hadi Alhamisi
2:30 asubuhi - 6:30 mchana
8:00 mchana - 11:30 jioni

Au wasiliana nasi kwa njia rahisi kupitia baruapepe ikunda.urio@goethe.de
Unaombwa kujiandikisha mwenyewe wakati wa muda vya kujiandikisha na siyo wakati wowote. Tunapokea malipo kupitia Benki na malipo kwa njia ya simu kupitia M-Pesa (Tanzania). Tafadhali fanya malipo baada ya kutibitisha kuwa umeandikishwa.
Kupitia mtihani wa kupima uwezo na mahojiano, tunaweza kufahamu hatua yako, kutengeneza malengo ya kujifunza pamoja na wewe, na kuchagua kozi nzuri kwa ajili yako.

Mtihani wetu wa kupima uwezo (kwa kuandika na kuongea) ni bure na hauhitaji kujiandikisha. Muda wa mtihani nje ya muda wa kawaida wa kujiandisha kwa miadi pekee

Tarehe: kwa miadi
Muda: saa 1 dk 30 (makadirio)
Ada: 30,000 TZS

Pima Kijerumani chako

Malipo ya Benki

Tanzania

National Bank of Commerce (NBC), Dar es Salaam
Akaunti namba: 012103020424
SWIFT: NLCBTZT

Ujerumani

Malipo kutoka nchi nyingine yanawezekana tafadhali wasiliana nasi - nassoro.nascov@goethe.de
  • Ada ya kozi haitarejeshwa endapo kozi itakuwa imeanza
  • Kughairisha ni sharti kufanywe kwa barua kwenda ofisi ya kozi za lugha
  • Ada ya 10% itatozwa endapo mwanafunzi atajiondoa kabla ya kuanza kwa kozi
1. mahitaji ya jumla
Mwanafunzi wa kozi anapaswa kuwa amefikisha miaka 18

2. Utaratibu wa Malipo
2.1. Baada ya kufanya maombi, mwanafunzi mtarajiwa atapokea taarifa ya awali ya uthibitisho. Taarifa hii itaonesha tarehe ya mwisho ya kufanya malipo kamili ya kozi.
2.2. Endapo malipo kamili hayatakuwa yamepokelewa hadi kufikia tarehe iliyotajwa, mwanafunzi mtarajiwa atapoteza nafasi ya kushiriki kozi. Ikitokea hivyo, Goethe-Institut (ikitajwa hapa kama "GI") itakuwa na haki juu ya ada.

3. Ada ya kozi
3.1. Ada ambayo mwanafunzi analazimika ni ile iliyopo kwenye orodha iliyotumika wakati wa kufanya maombi.
3.2. Endapo mwanafunzi anahitaji kubadilisha mpango wa masomo (kubadili tarehe za kozi), hatalazimika kulipa ada yoyote anapobadilisha kwa mara ya kwanza. Baada ya kubadilisha mpango kwa mara ya kwanza mwanafunzi atalipa 10% ya ada ya kozi kila mara atakapofanya mabadiliko.

4. Kujiondoa na kurejeshwa kwa ada
4.1 Masharti yafuatayo yatatumika endapo mwanafunzi wa kozi atashindwa kushiriki kwenye kozi: Endapo ataghairi katika kipindi cha wiki nne kabla ya kuanza kwa kozi, atatozwa ada inayolingana na 10% ya ada ya kozi. Endapo ataghairi katika kipindi cha wiki moja kabla ya kuanza kwa kozi, GI itakata ada inayolingana na 30% ya ada ya kozi.. Endapo ataghairi katika kipindi cha siku tatu za kazi kabla ya kuanza kwa kozi, GI itakata ada inayolingana na 50% ya ada ya kozi.. Endapo ataghairi katika kipindi ambapo kozi imeanza, hatarudishiwa ada na ada aliyolipa haitaweza kutumika kwa kozi inayofuata, bila kujali kama alikuwa ameanza kusoma au la.
4.2 Kughairisha ni sharti kufanywe kwa maandishi. Tarehe ya kughairisha itakuwa ni tarehe ya barua kupokelewa Goethe Institut.
4.3 Tamko la kujiondoa lazima lipelekwe kwa maandishi. Tarehe ya mwisho inaamuliwa na GI.

5. Mgawanyiko wa hatua za kozi/ukubwa wa darasa
5.1. Kupangiwa hatua ya kozi kutategemea matokeo ya mtihani wa kupima uwezo uliofanyika Goethe-Institut.
5.2. Kwa uchache kozi zetu zinakuwa na wanafunzi 6 na idadi ya juu ya wanafunzi katika kozi ni 20. Endapo idadi ya wanafunzi haitoshelezi siku ya kuanza kozi, tunayo haki ya kufuta au kuahirisha kozi. Inapotokea hivi tunawapa wanafunzi fursa ya kuhamia kozi nyingine au kurejeshewa kiasi kamili cha ada ya kozi. Tunasikitika kwamba kozi pekee tunazoweza kuendesha ni zile zilizokidhi idadi ya chini ya wanafunzi hadi kufikia tarehe ya mwisho ya kujiandikisha. Kuepuka kufutwa kwa kozi, jambo linalowezekana endapo wanafunzi watajiandikisha kabla ya kuanza kwa kozi, tunawashauri wanafunzi kwa mapenzi yao wenyewe kujiandikisha kabla ya terehe ya mwisho.

6. Wajibu wa wanafunzi
Wanafunzi wanawajibika kuzingatia kanuni za kozi na kanuni nyingine kama zilivyowekwa na Goethe-Institut.

7. Wajibu wa Goethe-Institut
Wajibu wa GI na wafanyakazi wake inakomea kwenye matukio ya makusudi ya uzembe mkubwa. Pia GI haitabeba dhamana yoyote ya kufutwa kwa huduma zake kunakotokana na dharura iliyo nje ya uwezo wake (mfano majanga ya asili, moto, mafuriko, vita, amri halali na hali nyingine zilizo nje ya uwezo wake).

Mawasiliano

Nassoro Nascov Nassoro Nascov
Mkuu wa Kitengo cha Lugha
Simu: +255 22 213 4800
nassoro.nascov@goethe.de
Ikunda Urio Urio Ikunda
Msaidizi wa kozi za Lugha
ikunda.urio@goethe.de
Juu