Washirika na wafadhili

Goethe-Institut Partners and Sponsors Photo: Goethe-Institut/Loredana La Rocca

Maendeleo ya miradi mikubwa hutegemea watu na taasisi ambao wako radhi kusaidia kazi hii njema, wakati huu kuliko wakati mwingine wowote. Rasilimali za ziada kutoka mashirika na wafadhili binafsi hutusaidia kutekeleza miradi ya kipekee yenye lengo la kuinua uelewa wa kimataifa na kutimiza wajibu.

Unaweza kusaidia kazi yetu kama mdhamini au msaidizi. Kwa mfano endapo ungependa kuhusika katika kusukuma mbele lugha ya Kijerumani kwa kusaidia mradi wa elimu au ushirikiano baina ya shule, au endapo unataka kukuza uelewa wa kina baina ya tamaduni kupitia programu za muziki, tamthiliya na sanaa za maonesho, tafadhali wasiliana nasi. Pamoja, tunaweza kufikia watu wengi na kujenga msingi wa uhusiano wa kudumu wa kirafiki.