Goethe-Zertifikat C1

Unafaa endapo unataka

  • kujiandaa kusoma kwenye chuo kikuu au taasisi ya elimu ya juu nchini Ujerumani
  • kuonesha uelewa mkubwa wa Kijerumani kwa ajili ya malengo ya kuajiriwa
  • kujiandaa kufanya kazi katika sekta ya afya
  • kuthibitisha kuwa umefaulu hatua ya C1
  • kupata cheti rasmi kinachotambulika kimataifa

Goethe-Zertifikat C1 ni mtihani wa Kijerumani kwa watu wazima. Unathibitisha kuwa watahiniwa wamepata ustadi zaidi wa kuongea lugha ya Kijerumani na unakidhi vigezo vya hatua ya tano (C1) katika ngazi ya hatua sita za uhadari zilizowekwa na Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR).

Kufaulu mtihani inamaanisha kuwa unaweza …

  • kuelewa kwa mapana maneno magumu na marefu ikiwa ni pamoja na maana zinazojitokeza bila kutajwa
  • kujieleza kwa ufasaha na usahihi bila kusitasita wala kuhitaji kusaka maneno,
  • kutumia lugha kikamilifu na kwa kunyumbulika kazini au katika jamii au wakati wa mafunzo au masomo yako
  • kutoa kauli zinazoeleweka wazi, zilizonyooka na zenye maelezo ya kina unapoongelea mada nzito
Tafadhali wasiliana na chuo kikuu, taasisi ya elimu ya juu au mtoaji wa kozi ya maandalizi kabla ya kuanza kwa kozi yako ili kubaini endapo mtihani wa Goethe-Zertifikat C1 utakidhi vigezo vya kukusamehe kufanya mtihani wa lugha kwa ajili ya kujiunga na chuo kwa wanafunzi wa kigeni.
 

Maandalizi

matini ya mazoezi

Mitihani ya mfano na matini ya kufanyia majaribio ambazo ni rahisi kutumia kukusaidia mtandaoni vinapatikana hapa

Maelezo zaidi

Mahitaji, yaliyomo katika mtihani na maelezo zaidi juu ya mtihani wa Goethe-Zertifikat C1 yanapatikana hapa: