Goethe-Test PRO: Deutsch für den Beruf

Goethe-Test PRO Deutsch für den Beruf Foto (Ausschnitt): Colourbox

Unafaa endapo unataka

  • Kwa mahitaji binafsi ya kazi yako: Tathmini ustadi wako wa lugha kiuhalisia / pambanua fursa za mafunzo na kozi zinazokufaa
  • Kwa makampuni: Pima ustadi wa lugha wa wafanyakazi na wanaoombaji kazi / tathmini mafanikio kutokana na mafunzo ya awali / tengeneza msingi sahihi wa hatua za baadaye za mafunzo

The Goethe-Test Pro – Bayana kwa dakika 60 tu

Iwe  kwa mahitaji binafsi ya kazi yako au kwa umahiri wa kampuni yako yote: Mafanikio siyo jambo la bahati. Mafanikio hutokana na uaminifu. Na uaminifu huimarika pale ambapo watu wote wanaongea lugha moja. Swali ni kwamba: Kijerumani chako ni kizuri kwa kiasi gani? Ni stadi gani za lugha zinazohitajika kwa wafanyakazi wako wa sasa na wajao?

Goethe-Test PRO: Kijerumani kwa wafanyakazi hutoa jibu kwa swali hilio. Mtihani wetu wa Kijerumani unaoendeshwa kwa nija ya kompyuta utafanya tathmini ya umahiri wa kusikia na kusoma kwa haraka na kwa uhakika mahali pa kazi.

Inarekebisha na kufahamisha

Goethe-Test PRO hutumia teknolojia ya hali ya juu kutathmini ustadi wa lugha wa mtu binafsi ndani ya dakika 60 hadi 90. Washiriki wote huanza mtihani katika hatua sawa. Kadri mchakato unavyoendelea, programu huchagua swali lifiatalo kutokana na jibu ulilotoa awali, na hivyo kufanya kiwango cha ugumu kubadilika chenyewe kulingana ustadi wako wa lugha. Hii inaondoa uwezekano wa kufeli: Matokeo ya mtihani na ripoti juu ya kiwango chako cha uhodari wa lugha hupatikana mara moja baada tu ya kumaliza mtihani - na hukupatia, kama unahitaji, msingi wa kufanya uamuzi, kwa mfano kuhusu mahitaji juu ya hatua za mafunzo ya ziada.

Goethe-Test PRO mtihani wa mtandaoni. Unaweza kufanywa katika moja ya vituo vyetu vilivyoenea duniani au kwenye ofisi za kampuni yako. Mtihani unatumia mbinu maarufu za huduma ya kupima lugha za kazi/biashara (BULATS) na msingi wake unatokana na Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR).

Jinsi ya kuwasiliana nasi

Je, unahitaji kujua kwa usahihi badala ya kukisia juujuu kuhusu ustadi wako wa lugha au ustadi wa wafanyakazi wako? Kama ndiyo usisite kuwasiliana nasi moja kwa moja! Tutakutumia mapendekezo ya ada kwa ajili yako na kukupa msaada wa maandalizi na kufanya mtihani.

Tutafurahi kukushauri juu ya mpango wa taratibu zinazofaa za kujifunza na kozi za lugha kwa makampuni.

Nini kingine ni muhimu kufahamu?


Toleo la mfano

Jionee mwenyewe sas, bila malipo:

Mawasiliano

Kufahamu zaidi au kupata maelezo kwa ajili yako, tafadhali wasiliana na:
 
nassoro.nascov@goethe.de
ikunda.urio@goethe.de