Her Hip Hop

Her Hip Hop © Hip Hop Asili Festival

Kikundi cha Hip-Hop cha akina dada wa kitanzania kilivyowezeshwa kujikita kwenye Soko la muziki Tanzania. Mapitio ya mafanyikio yatokanayo na mchango kutoka kwa Mfuko wa kuendeleza sanaa cha Ujerumani na Ufaransa.

Ni nadhara kusikia wakina mama wameunda kikundi cha muziki wa Hip-Hop kwa Tanzania. 
Ila mara hii kikundi cha wadada pekee cha Bongo Queens,  kilijitokeza nchini Tanzania kwa kuwakilisha Hip-Hop.
Wakina dada wa kikundi hicho walijikusanya kuanzia mwaka 2022 na 2023 kupitia mradi wa pamoja uliyopewa jina ya „ Her Hip - Hop Experience.

Mradi wa huu wa „Her Hip-Hop Expierence ulifanyikiwa kutokana na jithahda na ushirikiano wa balozi za Ujerumani na Ufaransa, vituo vya utamaduni za Ujerumani na Ufaransa, OKaa Mtaa Foundation cha Arusha, Uswazi Born Talents cha Dar es Salaam pamoja na mfuko wa ukuzaji utamaduni wa Ufransa na Ujerumani.

Akina dada wa Bongo Queens waliongozwa katika kujiimarisha katika fani ya Hip-Hop na wataalum wa muziki Carola Kinasha kutoka Tanzania, Julie Gomel kutoka Ufaransa na mshauri wa biashara ya muziki Pamela Owusu-Brenyah kutoka Ujerumani.

Washiriki wa mradi wenyewe walikuwa ni wanamuziki kutoka Arusha na Dar es Salaam. Wakiwa kama kikiundi waliweza kufunzwa na kuifahamu vyema baadhi ya vipengele muhimu za muziki ili kumudu ushindani wa soko la muziki.  Wakati wa mradi kikundi hicho kilijifunza uchezaji na umilkaji wa jukwaa, uimbaji kwa sauti, nyanja za masoko ya muziki na utambuaji wa nafasi katika kutekeleza kazi ya muziki hasa wa Hip-Hop hapa Tanzania.

Baada ya mafunzo na kilele cha mafunzo wa mradi wa Her Hip -Hop experience ilikuwa ni kutoa video nyimbo „Walete“ wa Bongo Queens, uliyotolewa kwenye Youtube na Spotify.
Pia Kikundi hicho kilialikwa kwenye toleo la tatu ya Tamasha ya Hip-Hop Asili Festival hapa Dar es Salaam, June 2023. Pia kama kikundi kilichofundwa vyema walialkiwa kwenye vituo kadhaa hapa Tanzania wajitambulisha kama kikundi na kibao chao “Walete”.

Mradi wa Her Hip Hop Experience na kikundi cha Bongo queens imeonyesha uwezo wa mikusanyiko kuleta matokeo mazuri na ya kuhamasisha washiriki na wafuatilaji kuleta mabadiliko na kuhoji mwendelezo wa uwezaji kwa njia tofauti.

Tufuatilie