Taarifa zaidi

Kurudi kwenda Goethe-Zertifikat B2

Moduli moja moja

Mtihani wa Goethe-Zertifikat B2 unajumuisha seksheni za kusoma, kusikiliza, kuandika na kuongea (seksheni ya kuongea hufanywa katika jozi).
Mtihani hufanyika katika vituo vilivyochaguliwa kwa njia ya kidijitali au karatasi. Viwango vinavyofanana vya usimamizi na tathmini huzingatiwa duniani kote.
 

Kusoma

Unasoma maandishi mbalimbali kama vile maudhui yaliyotumwa mtandaoni, makala za magazeti na majarida, mawazo na maelekezo. Unaweza kupata taarifa za msingi, maelezo muhimu, pamoja na mitazamo, maoni na kanuni.

Muda: dakika 65

Kuandika

Unajieleza na kutetea maoni yako kwa kuandika kwenye maudhui yanayotumwa mtandaoni juu ya mada ya kijamii ya wakati uliopo. Pia unaandika ujumbe rasmi katika muktadha wa kitaaluma.

Muda: dakika 75

Kusikiliza

Unasikia usaili, mihadhara, mazungumzo na kauli juu ya maisha ya kawaida ya kila siku pamoja na kusikiliza kutoka kwenye redio. Unaweza kunasa ujumbe wa msingi na maelezo muhimu.

Muda: dakika 40

Kuongea

Unatoa mfadhara mfupi juu ya mada iliyopendekezwa na kuongea na mshirika wako wa mazungumzo kuhusu mada hiyo. Pia unachangia hoja katika majadiliano.

Muda: dakika 15

Mahitaji

Goethe-Zertifikat B2 ni mtihani wa Kijerumani kwa vijana na watu wazima.

Mitihani ya Goethe-Institut hutolewa kwa yeyote anayependa. Watahiniwa huweza kufanya mtihani bila ulazima wa kufikisha umri wa chini unaohitajika au kuwa na uraia wa Ujerumani.
  • Umri wa chini wa miaka 15 unahitajika ili kuweza kufanya mtihani wa Goethe-Zertifikat B2 kwa vijana.
  • Umri wa chini wa miaka 16 unahitajika ili kuweza kufanya mtihani wa Goethe-Zertifikat B2 kwa watu wazima.
  • Ili kufanya mtihani wa Goethe-Zertifikat B2, ni sharti mtahiniwa awe na ujuzi wa lugha ya Kijerumani unaofikia kiwango cha  ngazi ya umahiri ya B2 kulingana na Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR).
  • Ili kufikia ngazi hii, watahiniwa wanapaswa wawe wamekamilisha vipindi  600 and 800 vya dakika 45 za masomo, kwa kutegemea ujuzi wake wao awali na mahitaji yao ya mafunzo.