Taarifa zaidi

Kurudi kwenda Goethe-Zertifikat C2: GDS

Tengeneza alama zako! Moduli

Mtihani wa Goethe-Zertifikat C2: Großes Deutsches Sprachdiplom unajumuisha moduli za kusoma, kusikiliza, kuandika na kuongea. Moduli ya kusikiliza hufanywa na mtahiniwa mmoja mmoja. Mtihani husimamiwa na kutathminiwa kwa njia ileile duniani kote.
 
Majaribio ya moduli ya kuandika yanayohusiana na dondoo za kazi za fasihi yametungwa kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Ludwig Maximilian, Munich.
 
Moduli nne zinaweza kusomwa kila moja peke yake au kwa pamoja, na vyeti vinne tofauti kwa kila moduli vikiwa sana na cheti kimoja kwa duru ya moduli zote.
Moduli za kusoma, kusikiliza, kuandika na kuzungumza hupimwa katika kituo cha mitihani.
 

Kusoma

Unasoma maandishi ya maelezo ya kweli, mawazo, taarifa na matangazo ya biashara na na kila mmoja anafanya zoezi tofauti. Unaweza kuelewa maandishi kwa urahisi, hata kama yanachanganya au magumu kueleweka kwa upande wa maudhui na lugha, na wakati huohuo kuelewa maana inayojitokeza bila kutajwa.

Muda: dakika 80

Kuandika

Unarudia kuandika sehemu za wasilisho fupi na kuandika maandishi yaliyojikita juu ya mada ya jumla au inayohusiana na utunzi wa vitabu katika mpangilio mzuri na mtindo unaokubalika kama barua kwenda kwa mhariri au mapitio ya kitabu. Kuna mada mbili za jumla na mada moja kwa kila kitabu kati ya vitabu viliwili kutoka kwenye orodha kwa ajili ya uchaguzi wako. Unashughulika juu ya mojawapo kati ya mada nne zinazoweza kutolewa.

Muda: dakika 80

Kusikiliza

Utasikia ripoti na taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari, mazungumzo yasiyokuwa rasmi na usaili wa kitaalamu katika uongeaji wa kiasili na kufanyia kazi mazoezi tofauti.

Muda: takribani dakika 35

Kuongea

Unatoa mhadhara juu ya mada ngumu zaidi kueleweka, mf. B. Utandawazi, ambapo unafafanua msingi wa sababu zako kwa namna tofauti-tofauti pale unapoulizwa. Katika majadiliano ya hoja shindani, unajadili mada nyingine kwa kutoa maoni yako, kujibu hoja kinzani na kujaribu kumshawishi mshirika wako wa mazungumzo akubaliane na mtazamo wako.

Muda: takribani dakika 15

Mahitaji

Goethe-Zertifikat C2: Diploma ya Juu ya Lugha ya Kijerumani ni mtihani wa Kijerumani kwa watu wazima.
 
Mitihani kutoka Goethe-Institut hutolewa kwa yeyote anayependa na inaweza kufanywa bila ya kujali kama watahiniwa wamefikisha umri wa chini unaohitajika na pia bila kujali kama wana uraia wa Ujerumani.
  • Ili kupata Cheti cha Goethe C2: Diploma ya Juu ya Lugha ya Kijerumani, inashauriwa mtahiniwa awe na umri wa kuanzia miaka 18.
  • Cheti cha Goethe C2: Diploma ya Juu ya Lugha ya Kijerumani inahitaji ustadi wa lugha kwa kiwango cha ngazi ya sita na ya juu zaidi ya umahiri (C2) kulingana na Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR).
  • Ili kufikia ngazi hii, watahiniwa wanapaswa wawe wamekamilisha walau vipindi 1000 vya dakika 45 za masomo, kwa kutegemea ujuzi wao wa awali na mahitaji yao ya mafunzo.