Taarifa zaidi

Kurudi kwenda Goethe-Zertifikat A2: Fit in Deutsch

Mahali pazuri pa kuanzia: seksheni za mitihani

Mtihani wa Goethe-Zertifikat A2: Fit in Deutsch unajumuisha seksheni za kusoma, kusikiliza, kuandika na kuongea.
Mitihani husimamiwa na kutathminiwa kwa njia ileile duniani kote.

Kusoma

Unasoma maandishi kama vile makala fupi za magazeti, baruapepe, matangazo ya biashara na matangazo ya kwenye mabango na kufanya uhariri wa maandishi hayo.

Muda: dakika 30

Kuandika

Unaandika ujumbe ambao unahusiana na mazingira yako ya karibu unapoishi.

Muda: dakika 30

Kusikiliza

Unasikiliza mazungumzo ya kawaida ya kila siku, matangazo na mahojiano ya redio, taarifa kwa njia ya simu na matangazo ya hadhara na kufanya uhariri wa taarifa hizo.

Muda: dakika 30

Kuongea

Unauliza maswali na kujibu maswali juu ya mambo yanayokuhusu wewe mwenyewe, unaongelea kitu fulani kuhusu maisha yako na unakubali au kupanga jambo fulani pamoja na mshirika wako wa maongezi.

Muda: dakika 15

Mahitaji

Goethe-Zertifikat A2: Fit in Deutsch ni mtihani wa Kijerumani kwa vijana wa umri kati ya miaka 12 hadi 16.
 
Mitihani ya Goethe-Institut hutolewa kwa yeyote anayependa na inaweza kufanywa bila kujali umri au utaifa.
  • Umri wa chini wa miaka 12 unahitajika ili kuweza kufanya Mtihani wa Goethe-Zertifikat A2: Fit in Deutsch.
  • Ili kufanya Mtihani wa Goethe-Zertifikat A2: Fit in Deutsch, ni sharti mtahiniwa awe na ujuzi wa lugha ya Kijerumani unaofikia kiwango cha  ngazi ya pili ya umahiri (A2) kulingana na Mfumo wa Pamoja wa Ulaya wa Marejeo ya Lugha (CEFR).
  • Ili kufikia ngazi hii, watahiniwa wanapaswa wawe wamekamilisha vipindi 200 hadi 350 vya dakika 45, kwa kutegemea ujuzi wao wa awali na mahitaji yao ya mafunzo.