Fedha na Ushuru

geöffnete Geldbörse auf einem Tisch © Goethe-Institut/ Gina Bolle

Ukiwa unaishi na unafanya kazi Ujerumani, unahitaji akaunti ya benki. Mwajiri wako huweka mshahara wako kwenye akaunti hiyo. Unatumia pesa zilizomo kwenye akaunti yako ya benki kulipia kodi ya nyumba na bili zako. Unaweza kutoa pesa kwenye mashine za kiotomotela.

Audio-Player: Artikel anhören

Artikel anhören

Finanzen und Steuern

Akaunti ya Benki

Kuna benki na taasisi za kuweka akiba mbalimbali. Nyingine zina matawi katika maeneo mbali mbali. Unaweza kwenda pale na kuzungumza na wahudumu. Pia kuna benki za mtandaoni. Hizi unaweza kutumia tu kupitia kwa mtandao. Mara nyingi, unalipia kiasi fulani cha ada ili uwe na akaunti. Kwa wanafunzi wa shule na vyuo, mara nyingi akaunti zao huwa bila malipo.

Kwa pesa ulizo nazo kwenye akaunti, benki au taasisi ya kuweka akiba hukupa riba. Kwa akaunti ya matumizi ya kila siku, hupata riba kidogo sana. Ukipenda kuweka akiba, unaweza kufungua akaunti ya akiba ya kila siku au akaunti ya akiba ya kawaida. Kwa aina hizi za akaunti, riba huwa ya juu kidogo ukilinganisha na akaunti ya matumizi ya kila siku.

Kufungua Akaunti

Ungependa kufungua akaunti? Kuna aina tofauti za akaunti. Akaunti ya kawaida ya benki huitwa “Girokonto”. Wakati mwingine benki inaweza kukataa kukupa akaunti hiyo, iwapo una kipato kidogo. Katika hali kama hiyo, benki inalazimika kukupa akaunti ya msingi. Kwa akaunti hii unaweza kufanya mambo ya natija kama: kuhamisha hela, kulipa kwa kadi, kuweka na kutoa hela. Mara nyingi hii ni akaunti ya amana,unaweza tu kutumia kiasi cha hela zilizopo kwenye akaunti.

Kwa akaunti yenye mkopo wa matumizi, unaweza pia kutoa hela hata kama akaunti haina hela. Benki hukukopesha hadi kiwango fulani. Lakini unalazimika kuirudishia benki hiyo hela pamoja na riba. Riba hizi mara nyingi huwa juu za sana.

Ili kufungua akaunti, unaweza kwenda katika tawi lolote la benki. Benki au taasisi ya kuweka akiba lazima ithibitishe utambulisho wako mwanzo. Kwa hivyo unapaswa kuonyeshana kitambulisho au pasipoti yako.

Kwa benki nyingi, unaweza pia kufungua akaunti kwa njia ya mtandao au posta. Kwa hili unaweza kutumia utaratibu wa uthibitisho wa utambulisho kupitia posta (Postident),unapata nyaraka kutoka kwa benki. Ukiwa na nyaraka hizo na kitambulisho au pasipoti yako, unaenda posta. Huko ndiko utambulisho wako utadhibitishwa. Wakati mwingine, unaweza kuhitajika pia kutoa cheti cha usajili wa makazi yako ili kufungua akaunti.

Huduma za Mtandaoni za Kibenki

Mambo mengi ya benki hufanyika kupitia kwa mtandao. Hili litarejelewa kama huduma za mtandaoni za benki. Waja wachache sana ambao huenda tena kwenye matawi. Waja wengi hutumia mpango wa simu. Wakati wa kufungua akaunti, waeleze kuwa ungependa kutumia huduma za mtandaoni au nyumbani. Kwa njia hii unaweza kufanya uhamisho wa fedha kwa haraka na urahisi. Kwa mfano unapolipa bili. Unachohitaji ni taarifa za akaunt, ni nani anapokea pesa? IBAN ni ipi? Kwa uhamisho wa mara kwa mara, kama vile kodi ya nyumba, unaweza kuweka maagizo ya kudumu.

Tangu 2014, katika nchi nyingi za Ulaya kuna mfumo wa malipo wa SEPA. Kwa mfumo huu unaweza kuhamisha pesa za euro kwa urahisi. Unahitaji IBAN na BIC. Hizi ni safu za tarakimu na herufi. IBANna BIC hupatikana kwenye kadi yako ya benki, kwa mfano.

Je, ungependa kununua bidhaa mtandaoni? Kuna njia mbalimbali za kulipia, unaweza kutumiwa bili na kuhamisha pesa. Unaweza pia kulipa kwa kutumia kadi ya debit au ya mkopo. Kuna pia huduma za malipo kama vile PayPal au Klarna. Waja wengi Ujerumani wana akaunti ya PayPal. Kwa akaunti hii unaweza pia kutuma pesa kwa wandani kwa urahisi..

Kadi za Fedha

Kuna aina mbalimbali za kadi za fedha: kadi ya matumizi ya kila siku, kadi ya mkopo au kadi ya malipo ya moja kwa moja (kwa mfano: MasterCard, Visa). Kadi ya Giro ilijulikana zamani kama kadi ya EC. Waja wengi bado hutumia jina hili. Gharama za kadi hutofautiana baina ya benki. Kadi moja huwa bila malipo mara nyingi. Benki au taasisi ya kuweka akiba hukutumia kadi kwa posta. Unapaswa kutia sahihi kwenye kadi hiyo. Baada ya siku chache, utatumiwa namba ya siri kwa posta, yaani nambari ya PIN. Unapaswa kuikumbuka.

Kwa kutumia kadi ya matumizi ya kila siku, (Debit-Karte) au kadi ya mkopo, unaweza kutoa pesa kwenye mashine yoyote kiotomotela. Unahitaji namba ya siri kila wakati. Benki na mashine zingine hutoza ada na zingine hazitozi. Wakati mwingine unaweza pia kutoa pesa kwenye kaunta ya duka kubwa.

Unaweza pia kutumia kadi ya matumizi ya kila siku kulipa katika maduka na mikahawa. Mara nyingi, debit-kadi au kadi ya mkopo pia hukubalika. Tahadhari: Ujerumani si kila mahali unaruhusiwa kulipa kwa kadi. Wakati mwingine mikahawa, vibanda au maduka madogo hukubali pesa taslimu tu.

Umepoteza kadi yako au imeibiwa? Ifungie haraka iwezekanavyo. Piga simu ya dharura ya kufungia kadi kwa nambari 116116.

Mshahara na Gharama za Maisha

Mwajiri wako hukulipa mshahara. Mara nyingi mnakubaliana mshahara wa mwaka mzima kabla ya makato. Lakini sio pesa hizo zote huingia kwenye akaunti yako. Sehemu ya pesa hizo hutolewa kwa ajili ya bima ya jamii ya lazima. Pia serikali huchukua kodi ya mapato kutoka kwa mshahara wako. Mshahara halisi ni kiasi kinachobaki. Mwajiri wako huwa anakutumia kiasi hicho kila mwezi kwenye akaunti yako. Hakikisha kuwa pesa hizo zinakutosha kwa maisha yako. Unahitaji pesa kwa ajili ya nyumba, chakula, burudani na mengine mengi. Soma maelezo zaidi katika maandiko yetu ya taarifa kuhusu Bima na Kuanza kazi.

Msaada wa Kifedha

Akraba, waja wenye kipato kidogo na waja wenye maumbile maalum hupata msaada wa kifedha kutoka kwa serikali. Soma maelezo zaidi katika taarifa yetu kuhusu “Maisha na Watoto” na “Maisha na Ulemavu”.

Ushuru

Ujerumani kuna wajibu wa kulipa ushuru. Hii ina maana kuwa waja wote wanaofanya kazi hulipa ushuru wa mapato yao. Huu ni ushuru unaotolewa kwenye mshahara. Unapewa namba ya ushuru kutoka kwa Wizara ya Fedha na namba ya ushuru ya utambulisho kutoka kwa mamlaka kuu ya ushuru ya shirikisho. Hii ni namba ya tarakimu 11. Pia unayo kadi ya ushuru ya kielektroniki (ELStAM). Hii hutumwa moja kwa moja na Wizara ya Fedha kwa mwajiri.

Wewe ni mfanyakazi? Basi mwajiri wako hutuma ushuru wa mapato kwa Wizara ya Fedha. Huna haja ya kufanya chochote. Wewe ni mwenyekampuni? Hata wajasirimali wanalazimika kulipa ushuru wa mapato. Hili ni gumu zaidi kidogo. Wajasirimali wanafanya malipo ya mapema kwa Wizara ya Fedha. Kila mwaka, wanafanya tamko la ushuru. Baada ya hapo, wanaweza kulipa zaidi au kurejeshewa pesa.

Kiwango cha ushuru wa mapato kinategemea mshahara. Wanaopata zaidi wanalipa zaidi. Wanaopata kidogo wanalipa kidogo. Pia daraja la ushuru lina athari. Kwa mfano, waliooa au walio na watoto hulipa ushuru kidogo.

unalipa ushuru wa kanisa. Kampuni hulipa ushuru wa biashara kwa jiji au halmashauri.

Hata wafanyakazi hufanya tamko la ushuru wa mapato kila mwaka. Kwa njia hii, wanaiambia Wizara ya Fedha ni kiasi gani walipata. Pia wanaeleza ni matumizi gani waliyo nayo. Wafanyakazi mara nyingi hurudishiwa pesa na Wizara ya Fedha baada ya tamko hilo. Unaweza kufanya tamko la ushuru mwenyewe, kwa mfano kupitia tovuti ya ELSTER ya Wizara ya Fedha. Pia unaweza kusaidiwa na mshauri wa ushuru. Lakini huduma hiyo huwa inatozwa ada.

Bima

Ujerumani kuna aina nyingi za bima. Baadhi ni za lazima, zingine ni hiari. Bima muhimu ni ya pensheni. Ili uwe na fedha za kutosha unapostaafu, kuna pensheni ya kisheria. Lakini mara nyingi haitoshi. Bima ya binafsi ya uzeeni mara nyingi huwa na faida. Soma zaidi kuhusu hili kwenye maandiko yetu ya taarifa “Bima

Hati Muhimu

Hifadhi vizuri hati muhimu zinazohusiana na fedha zako. Hali kadhalika, hifadhi vizuri hati zinazohusiana na utambulisho wako, kama vile cheti cha bima ya jamii au pasipoti yako. Hili linahusu pia vyeti vya binafsi kama vile cheti cha kuzaliwa au cheti cha ndoa. Hifadhi kwa usalama pia vyeti vya shule na vya ajira.

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Tufuatilie