Ndoa

Hände mit Ringen © Goethe-Institut

Katika nchi nyingi waja hufunga ndoa katika Mamlaka ya usajili wa ndoa. Hii ni ndoa inayotambuliwa na serikali. Hali ni vivyo hivyo nchini Ujerumani. Ni kwa njia hii tu ndoa inakuwa halali. Baada ya hapo, mja anaweza pia kufunga ndoa ya kanisa. Ili kufunga ndoa, wote wawili sharti wawe na angalau umri wa miaka 18.

Audio-Player: Artikel anhören

Artikel anhören

Heirat

Ndoa kwa Wote

Nchini Ujerumani, kuna wanandoa wengi wanaoishi pamoja bila kuoana. Hali hii ipo pia katika akraba zilizo na watoto. Kila mja ana uhuru wa kuamua.

Tangu tarehe 1 Oktoba 2017, hata wanandoa wa jinsia moja, yaani mwanaume na mwanaume au mwanamke na mwanamke, wanaweza kuoana nchini Ujerumani. Wana haki na wajibu sawa. Hii ina maana kuwa, wanaruhusiwa kuasili watoto. Wanaruhusiwa kuchukua jina la mwenza wao. Wanalazimika kuungana na kuauniana.

Hati Muhimu

Ungependa kufunga ndoa nchini Ujerumani? Jisajili katika Mamlaka ya usajili wa ndoa ya mahali unapoishi. Utahitaji hati kadhaa: kitambulisho chako au pasipoti, cheti chako cha kuzaliwa, cheti cha usajili wa makazi, na cheti cha uwezo wa kufunga ndoa. Je, una watoto? Basi lazima ulete pia hati za watoto hao. Uliza katika Mamlaka ya usajili wa ndoa iwapo unahitaji hati nyingine zaidi.

Sharti utafsiri hati zako kutoka kwa nchi yako ya asili kwenda lugha ya Kijerumani. Mkalimani aliyeidhinishwa sharti atie sahihi kuthibitisha kuwa tafsiri hizo ni sahihi. Ni sharti athibitishe tafsiri hizo kwa njia rasmi.

Baada ya kufunga ndoa, utapokea hati mpya katika Mamlaka ya usajili wa ndoa: Cheti cha ndoa. Ukipenda, unaweza pia kupewa kitabu cha akraba kilicho na taarifa za familia yako.

Je, tayari umefunga ndoa katika nchi yako ya asili? Unaweza kutambua cheti cha ndoa ya nje katika Mamlaka ya usajili wa ndoa nchini Ujerumani. Uliza haya katika Mamlaka ya usajili wa ndoa ya jiji lako.

Sherehe ya Harusi

Waja wengi huandaa sherehe kubwa ya harusi. Bibi harusi na bwana harusi huwakaribisha wageni wengi. Harusi hiyo huhudhuriwa na jamaa kama vile wazazi, ndugu, babu na bibi, mashangazi, wajomba, binamu wa kike na wa kiume. Na bila shaka, wandani wa karibu pia hualikwa. Mara nyingi pia huja wenza wa kazi. Kawaida, harusi nchini Ujerumani huhudhuriwa na wageni takriban 100. Kwa hivyo sherehe hazihusishi waja wengi kama ilivyo katika baadhi ya nchi zingine.

Kuna chakula, muziki na ngoma. Bibi harusi na bwana harusi hucheza dansi ya pamoja huku wageni wote wakiwatazama. Wanakata keki ya harusi pamoja. Wakati mwingine, kuna michezo kwa ajili ya bibi na bwana harusi. Mwanamke huvaa mara nyingi gauni jeupe la harusi. Wapenzi wengi hununua pete za ndoa. Wageni huleta zawadi. Mara nyingi, wao hutoa hela kama zawadi. Wageni wanaweza pia kuwauliza wanandoa mapema wanapenda zawadi gani.

Uunganishaji wa Familia

Mumeo au mkeo bado yuko katika nchi yako ya asili? Unaweza kumleta nchini Ujerumani. Kwa hili, utahitaji kibali cha ukaazi. Hili linahusu tu wanandoa na watoto wao walio chini ya miaka 18. Hii huitwa uunganishaji wa akraba au uunganishaji wa wanandoa. Wataalamu fulani wa kimataifa pia wanaruhusiwa kuwaleta wazazi na wakwe zao nchini Ujerumani. Hili linatumika iwapo ulipokea kibali chako cha ukaazi baada ya tarehe 1 Machi 2024.

Kuna masharti maalum kwa hili. Sharti uweze kuihudumia akraba yako. Akraba yako sharti iwe na nafasi ya kuishi katika nyumba yako. Unahitaji bima ya afya. Mume au mke wako anahitaji kuwa na maarifa ya msingi ya Kijerumani. Anatakiwa kuwa na cheti cha lugha. Kupitia kwa cheti hiki inaonyesha kuwa ana kiwango cha lugha angalau A1. Watoto walio chini ya miaka 16 hawahitaji mtihani wa lugha ya Kijerumani.

Kutengana na Talaka

Ndoa yako haiko vizuri tena? Mnapingana sana? Jaribuni kwanza ushauri wa ndoa au tiba ya wanandoa. Wakati mwingine, hilo linaweza kuauni.

Lakini wakati mwingine kuna sababu za kutengana au kutalikiana. Talaka si jambo rahisi. Kwanza, sharti muishi mkitengana kwa muda wa mwaka mmoja. Tafuta ushauri. Ofisi za ushauri hutoa msaada kuhusu masuala ya kisheria au masuala yanayohusu watoto, kwa mfano watoto watakaa na nani au ni nani atatoa kiasi gani cha hela.

Maswali Ya Mara kwa Mara

Tufuatilie