"Shule: Washirika kwa ajili ya siku zijazo" (PASCH)

 • Initiative „Schulen: Partner der Zukunft“ © Kai Uwe Oesterhellweg
 • Initiative „Schulen: Partner der Zukunft“ © Kai Uwe Oesterhellweg
 • Initiative „Schulen: Partner der Zukunft“ © PASCH-net
 • Initiative „Schulen: Partner der Zukunft“ © Kai Uwe Oesterhellweg
 • Initiative „Schulen: Partner der Zukunft“ © Keller
 • Initiative „Schulen: Partner der Zukunft“ © PASCH-net
 • Initiative „Schulen: Partner der Zukunft“ © Jens Sauerbrey

Mradi wa "Shule: Washirika kwa ajili ya siku zijazo" (PASCH) unatengeneza mtandao wa kimataifa wa zaidi ya shule 2,000 zilizo na uhusiano mahsusi na Ujerumani. Goethe-Institut inatoa msaada kwa takribani shule 600 za PASCH katika mfumo wa elimu ya taifa kutoka zaidi ya nchi 100.

Mradi wa "Shule: Washirika kwa ajili ya siku zijazo" (PASCH) ulizinduliwa Februari 2008 na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani. Mradi wa PASCH unaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na unatekelezwa kwa ushirikiano na Wakala Mkuu wa Shule za Nje (ZfA), Goethe-Institut, Ofisi ya Ushirikiano wa Kitaaluma ya Ujerumani na Ofisi ya Ushirikiano wa Kitaaluma ya Kamati ya Kudumu ya Wizara ya Elimu na Mambo ya Utamaduni ya Länder ya Jamhuri ya Shikisho la Ujerumani.

Kanuni na malengo

PASCH inaratibiwa kulingana na kanuni kuu nne:
 • kufikia matarajio kupitia elimu,
 • kukuza uelewa kupitia lugha mbalimbali,
 • kujifunza lugha na kupata elimu na
 • kukabili pamoja matatizo yajayo kama jumuiya ya wasomi kimataifa

Mradi wa "Shule: Washirika kwa ajili ya siku zijazo" (PASCH) ulizinduliwa Februari 2008 na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani. (PASCH) unatengeneza na kuimarisha mtandao wa kimataifa wa zaidi ya shule 2,000 zilizo na uhusiano mahsusi na Ujerumani. Goethe-Institut inatoa msaada kwa takribani shule 600 za PASCH katika mfumo wa elimu ya taifa kutoka zaidi ya nchi 100.

Mradi wa PASCH unaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na unatekelezwa kwa ushirikiano na Wakala Mkuu wa Shule za Nje (ZfA), Goethe-Institut, Ofisi ya Ushirikiano wa Kitaaluma ya Ujerumani na Ofisi ya Ushirikiano wa Kitaaluma ya Kamati ya Kudumu ya Wizara ya Elimu na Mambo ya Utamaduni ya Länder ya Jamhuri ya Shikisho la Ujerumani.

Mtandao wa shule za Kijerumani nchi za nje na shule zinazotoa Cheti cha Lugha ya Kijerumani unaimarishwa. Vilevile, ushirikiano na mashule unachagizwa na mtazamo wa kukifanya Kijerumani kuwa lugha ya kigeni katika mfumo wa taifa wa elimu. Kwa kuongezea, kunatolewa ufadhili wa kuhudhuria kozi nchini Ujerumani pamoja na fursa za kutembeleana baina ya mashule na programu za undugu baina ya shule za Ujerumani na shule kutoka sehemu nyingine duniani.

Malengo ya PASCH

Mradi umebuniwa ili kuamsha na kukuza hamu na shauku waliyonayo vijana juu ya Ujerumani ya sasa, jamii ya Kijerumani na lugha ya kijerumani. Mtandao wa kimataifa wa undugu baina ya shule wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani unaundwa; mashule yanakuwa sehemu ya juiya ya kimataifa ya wanafunzi kupitia shughuli za pamoja na kutembeleana. 

Mradi wa PASCH unatoa kozi za kuvutia za mafunzo zinazosaidia kuwapa wanafunzi na walimu sifa zitakazowafaa kwa muda mrefu, na hivyo kujenga msingi wa stadi ambazo vijana watazihitaji ili kujiunga na masomo nchini Ujerumanina kwa ajili ya maisha yao ya baadaye. Vilevile mradi umekusudia kuimarisha urafiki hai na wa muda mrefu na ujerumani na kuzishawishi shule, walimu na wanafunzi kushirikisha mawazo yao kwa uwazi baina yao na kufanya kazi pamoja. Pia, PASCH inafungamana na miradi mingine ya uhusiano wa utamaduni na sera za elimu kimataifa kama vile huduma ya kujitolea ya “Kulturweit”.

Wajibu na shughuli za Goethe-Institut

Goethe-Institut hutoa msaada kwa zaidi ya shule 600 kwa kuzisaidia kuingiza au kupanua wigo wa ufundishaji wa lugha ya Kijerumani katika mitaala yao. Pia huwapa walimu mafunzo ya ziada juu ya mbinu na maarifa ya kutoa kozi za lugha, na kuziwezesha shule kupata matini ya kisasa ambayo ni rahisi kutumia katika kujifunza na kufundisha masomo ya utamaduni na lugha. Ndani ya utaratibu wa mradi, Goethe-Institut hutuma pia wataalamu wa ufundishaji kusaidia shule zilizomo kwenye mradi sehemu mbalimbali duniani. Programu za vijana huendeshwa nchini Ujerumani kwa wanafunzi kutoka shule washirika, zikiwasaidia kuboresha ustadi wao wa lugha, kuendeleza stadi zao za kitamaduni na kupata uzoefu mzuri wa Ujerumani na utamaduni wake.
The www.pasch-net.de tovuti imegawika katika sehemu tatu:
 • Eneo kuu
 • Eneo la walimu
 • Eneo la Wanafunzi
Eneo kuu

Eneo kuu natoa taarifa kuhusu taasisi washirika na shughuli zao. Shughuli hizi zinajumuisha miradi midogo ilimo katika utaratibu wa mradi wa PASCH, blogu za wafanyakazi kutoka ofisi mbalimbali za kikanda duniani, kozi za PASCH kwa vijana nchini Ujerumani na jukwaa ambalo mashule huweza kupata shule za kuanzisha undugu kutoka nchi mbalimbali. Ramani ya kuvutia ya ulimwengu inaonesha mtandao wa shule washirika, na shule washirika huweka kwa kifupi taarifa zinazotoa picha juu yao.

Eneo la walimu

Katika eneo hili, walimu huweza kupata dhana au fikra juu ya kutumia PASCH-net katika vipindi vyao vya somo la Kijerumani, kupakua matini ya kufundishia na kupata taarifa kuhusu mbinu na maarifa ya ufundishaji. Jukwaa la mafunzo la PASCH huwawezesha walimu kufanya maandalio kwa njia ya mtandao au kutumia kozi zilizopo.

Kama jamii, walimu huweza kushirikisha matini yao au kupata washirika kwa ajili ya kutimiza fikra juu miradi yao. Kupitia jumuiya, jukwaa la mafunzo na blogu, walimu huweza kutekeleza miradi ya kimataifa kama vile magazeti kwa njia ya mtandao pamoja na vipindi vya sauti.

Kwenye jukwaa la mafunzo la PASCH, PASCH-net hutoa kozi za ziada ya mafunzo zinazofundishwa kwa njia ya mtandaokwa walimu. Kupitia kozi ya mtandaoni ya PASCH-net-Führerschein, walimu hujifunza kuhusu manufaa ya tovuti hiyo katika vipindi vyao vya lugha ya Kijerumani, kama vile jumuiya, jukwaa la mafunzo na gazeti la kimataifa la PASCH kwa mashule. Kupitia kozi ya mtandaoni ya Moodle-Führerschein wanajifunza jinsi jukwaa la mafunzo la PASCH, linalotumia programu za Moodle, linavyoweza kutumika katika vipindi vya shule au wakati wa kozi za mafunzo ya ualimu.

Mawasiliano: lernplattform@pasch-net.de

Eneo la wanafunzi

Wanafunzi wanaosoma lugha ya Kijerumani kwenye shule za PASCH huweza kushirikishana mawazo na mitazamo yao na wanafunzi kutoka jumuiya nyingine. wanaweza pia kutuma machapisho, picha na video, kujiunga katika vikundi na kutengeneza jukwaa la majadiliano.

Mashindano na miradi huwapa moyo vijana kushiriki. Machapisho katika hatua tofauti za ugumu wa lugha hutoa taarifa kuhusu Ujerumani, ikiwemo uwezekano wa kwenda huko masomoni.

Mada za majadiliano, shughuli na michezo ya lugha kwa wanafunzi wa Kijerumani.

Yeyote anayetaka kuchangia kwenye jumuiya au jukwaa la kujifunza la PASCH-net anapaswa kujisajili na kuingia kwa kutumia anuani ya baruapepe na nenosiri. Mawasiliano: service@pasch-net.de
Mtandao wa PASCH unajumuisha zaidi ya shule 2,000 kutoka duniani kote. Goethe-Institut inatoa msaada kwa zaidi ya shule 550 katika mfumo wa taifa wa elimu kutoka zaidi ya nchi 100. Kupitia utaratibu wa mradi wa "Shule: Washirika kwa ajili ya siku zijazo ”, shule hizi zimeingiza au kupanua wigo wa kufundisha lugha ya Kijerumani katika mitaala yao. Kwa kiasi kikubwa, Kijerumani kinafundishwa kama lugha ya pili ya kimataifa katika mashule.

Vilevile mtandao wa PASCH unajumuisha takribani shule 140 za Kijerumani nchi za nje zinazosaidiwa na Wakala Mkuu wa Shule Nchi za Nje (ZfA), shule 27 zinazotilia mkazo Kijerumani, pamoja na takribani shule 1,100 za kitaifa zinazotoa Cheti cha Lugha ya Kijerumani kutoka  Kamati ya Kudumu ya Wizara ya Elimu na Mambo ya Utamaduni ya Länder ya Jamhuri ya Shikisho la Ujerumani.

Picha za shule