Kazi & Taaluma
Je, una mpango wa kuishi na kufanya kazi Ujerumani? Hapa unaweza kupata majaribio ya kufanya bila malipo ili kuboresha Kijerumani chako kwa ajili ya kazi – kuanzia ngazi A1 hadi C2. Majaribio haya yatakusaidia pia kujua hali halisi ya kufanya kazi Ujerumani kwa mwajiri wa Kijerumani. Unatakiwa kuzingatia nini kabla ya usaili wa kazi? Kwa wastani watu hufanya kazi muda wa saa ngapi kwa juma? Utapata majibu ya maswali haya, na maswali zaidi kuhusiana na mahali pa kazi, katika video kutoka kwa watu ambao tayari wanafanya kazi Ujerumani.