Watoto & Vijana

Je, ungependa kuwa na uwezo wa kutuma maoni kwa Kijerumani kwenye mtandao wa TikTok na Instagram? Je, unafurahia kucheza michezo ya kuvutia mtandaoni? Au kuangalia filamu za Kijerumani? Kama ni hivyo, kufanya mazoezi kupitia Goethe-Institut ndiyo chaguo lako! Tumetengeneza app na michezo, pamoja na video na kuchagua zaidi ya filamu 100 kwa ajili yako. Pia, tunakuonesha majaribio ya kuvutia sana chuo chetu kikuu cha kidijitali kwa watoto na vijana wadogo.

Zwei Kinder flüstern sich etwas zu und lachen. © Goethe-Institut, Getty Images

  • Jukwaa la watoto

    Chuo Kikuu Cha Kidijitali Cha Watoto

    Ni kwa namna gani magari yanayojiendesha yenyewe hujiongoza? Kwanini ganda la konokono hutoa sauti nikilishika karibu na sikio langu? Kwanini ninahitaji kulala? Dunia imejaa maswali. Na tuna majibu – yaliyofafanuliwa wazi na bila malipo. Professor Einstein na Sophie Schlau wanatazamia kukutana na wewe!

    KinderUni Foto: © Goethe-Institut Foto: © Goethe-Institut

  • Chuo Kikuu Cha Kidijitali Cha Vijana Wadogo

    Jukwaa la vijana

    Kuna mwonekano gani anga za mbali? Umeme unatoka wapi? Na roboti hufanyaje kazi? Kama mwanafunzi katika  chuo kikuu chetu cha kidijitali cha vijana wadogo, utajifunza majibu ya maswali haya na maswali mengine, na papo hapo kuboresha Kijerumani chako , bila malipo. Chuo kikuu cha awali kinafaa zaidi kwa ngazi A1/A2 na A2/B1. 

    JuniorUni Foto: © Goethe-Institut Foto: © Goethe-Institut

  • Mitandao ya kijamii

    Jifunze Kijerumani kwenye mtandao wa TikTok na Instagram

    Karibu kwenye jumuiya yetu! Alex kutoka Berlin na wageni kutoka duniani kote  wanakusubiri kwenye chaneli zetu za TikTok na Instagram. Jifunze mambo yote kuhusu lugha ya Kijerumani, jipatie ufahamu wa maisha ya kila siku Ujerumani na katika nchi nyingine pamoja na kushirikisha uzoefu wako kwa wengine.

    Learn German on TikTok and Instagram © Goethe-Institut © Goethe-Institut

  • App ya kujifunzia

    Ifahamu Ujerumani

    Kwa Kijerumani au lugha utakayochagua: App hii isiyo ya kulipia itakufundisha mambo yote kuhusu Ujerumani – hali halisi ya kuishi hapa na kuhusu historia ya nchi hii. Utapata idadi ya kutosha ya mazoezi shirikishi, mtihani wa majaribio na video za kukusaidia kufanya mazoezi ya Kijerumani kwa urahisi na bila malipo – nyumbani au njiani.

    Deutschland.Kennen.Lernen Grafik: © Goethe-Institut Grafik: © Goethe-Institut

  • Taarifa na dondoo

    Mein Weg nach Deutschland

    Je, una mpango wa kuhamia Ujerumani? Kama ni hivyo, umekuja mahali sahihi. Pata taarifa muhimu kuhusu kuishi na kufanya kazi Ujerumani – kwa Kijerumani (ngazi A1 hadi B2) au kwa lugha utakayochagua – kupitia maandishi, video na ramani.

    Das Gesicht einer jungen dunkelhaarigen Frau ist vor dem Brandenburger Tor zu sehen im Sonnenlicht. © Alina Holtmann / Maridav © Alina Holtmann / Maridav

  • YouTube

    Jifunze Kijerumani na Ida

    Habari! Mimi ni Ida, mwalimu wako wa Kijerumani kupitia YouTube. Nitakusaidia kujifunza sarufi na maneno mapya, pamoja na  kukupatia dondoo za kuishi Ujerumani. Ni rahisi sana kuelewa video zangu endapo tayari unaweza kuongea Kijerumani kidogo (ni nzuri zaidi kwa ngazi A2 hadi B1) na hakuna malipo yoyote.

    Ida aus 24h Deutsch mit einem Mikrofon in der Hand Foto: © Goethe-Institut Foto: © Goethe-Institut

  • Mchezo wa mtandaoni

    Picha ya kuchora iliyopotea

    Picha ya kuchora iliyokuwa makumbusho imepotea. Wasaidie polisi na kuipata picha pamoja na rafiki zako Anna na Basti. Alama zako zitakuonesha ni kiasi gani tayari unafahamu Kijerumani.
    Mchezo wa kielimu kwa watoto wa miaka 7 hadi 10 katika ngazi ya kwanza ya A1.1.

    Screenshot vom Computerspiel „Das Bild ist weg!“ Grafik: © Goethe-Institut Grafik: © Goethe-Institut

  • App ya mchezo

    Jiji la maneno

    Endapo tayari unaweza kuongea Kijerumani kidogo na unapenda kujifunza maneno mapya kwa njia inayovutia zaidi, pakua app hii ya mchezo bila malipo! Inafaa zaidi kwa ngazi A1/A2. Utajifunza msamiati mpya kwa kiasi kikubwa na kuweza kulinganisha maelezo uliyoandika na yale ya wachezaji wengine.

     © Goethe-Institut © Goethe-Institut

  • App ya kujifunzia

    Mkufunzi wa Kijerumani A1

    Ninawezaje kuhesabu au kutaja muda kwa Kijerumani? Chakula hiki kinaitwaje? Ninasemaje tafadhali na asante? Hii app kwa ngazi A1 ni njia muhimu sana ya kuanza kujifunza Kijerumani bila malipo. Mkazo zaidi umewekwa katika kusikiliza, kusoma, kuandika na kujifunza maneno muhimu ya kuanzia.

    Deutschtrainer A1 Grafik: © Goethe-Institut Grafik: © Goethe-Institut

Tufuatilie