Maisha ya Kila Siku
Je, una mpango wa kukaa kwa muda mrefu kidogo Ujerumani – pengine hata kuhamia na kuishi au kufanya kazi huko? Wigo wetu mpana wa bila malipo wa majaribio, app na filamu unakusaidia katika kuboresha Kijerumani chako katika ngazi zote – kuanzia A1 hadi C2 kukuweka tayari kwa maisha ya kila siku Ujerumani. Kuanzia zoezi la kutafuta nyumba ya kupanga hadi kununua chakula, utajipatia stadi muhimu za mawasiliano kupitia washiriki kutoka katika jumuiya yetu ya wanaojifunza ambao tayari wamepiga hatua.