Kuongea Lugha za Kigeni

Kinderzeichnung © Goethe-Institut/ Simone Schirmer

Mja anayeweza kuzungumza vizuri zaidi ya lugha moja hupata faida nyingi katika maisha ya kila siku na kazini. Waja wanaofahamu lugha nyingi hujifunza mengi kuhusu tamaduni nyingine. Wana uelewa wa mwingiliano wa kitamaduni na wanaweza kuelewa mitazamo ya wengine kwa urahisi zaidi. Wanaweza kushiriki kikamilifu zaidi katika jamii.

Audio-Player: Artikel anhören

Artikel anhören

Mehrsprachigkeit

Faida za kuongea lugha za kigeni

Nchini Ujerumani wanaishi waja wengi kutoka nchi nyingine. Hawa ni zaidi ya asilimia 20 ya wakazi wote. Waja wengi wanaohamia Ujerumani hujifunza Kijerumani kama lugha ya pili au lugha ya kigeni. Lugha ya Kijerumani ni ya natija kwao. Wanaweza kuwasiliana na waja wengine. Wanaweza kupata kazi kwa urahisi zaidi. Wanaweza kuelewa vizuri zaidi utamaduni wa Kijerumani. Lakini pia lugha yao ya asili ni ya natija.

Kukuza Lugha ya Kijerumani

Lugha ya Kijerumani ni ya natija sana kwa waja wazima na watoto. Kwa kutumia lugha hiyo wanaweza kuwasiliana kwa urahisi zaidi. Wanaweza kupata wandani kwa urahisi sana. Waja wazima wanahitaji Kijerumani kwa ajili ya kazi na shughuli za kila siku, kwa mfano wakati wa kununua bidhaa au wanapokwenda ofisi za serikali. Katika ofisi nyingi taarifa huwasilishwa kwa lugha mbalimbali. Pia kuna wakalimani wa kuauni. Wao huzungumza Kijerumani na lugha ya asili ya mja. Wanaweza kutafsiri ikiwa huwezi kueleza au kuelewa jambo fulani. Watoto wanahitaji Kijerumani kwa ajili ya shule. Lugha hufunzwa kwa kusikiliza, kudurusu, kuzungumza na kuandika. Waja wazima wanaweza kuhudhuria kozi ya ujumuishaji au kozi nyingine za Kijerumani. Taarifa zaidi zinapatikana katika maandiko yenye kichwa „Kozi ya Ujumuishaji“.

Unahitaji kuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na lugha hiyo na nafasi nyingi za kufanya mazoezi. Ni vyema kutumia lugha ya Kijerumani mara kwa mara. Mazingira halisi kama sokoni ni bora zaidi. Wasiliana sana na waja wanaozungumza Kijerumani kikiwa lugha ya mama.

Watoto hujifunza Kijerumani mara nyingi kupitia mawasiliano, michezo na watoto wengine na watu wazima, kwa mfano kwenye kituo cha malezi ya watoto au shuleni. Watoto hawa hukua wakifahamu lugha zaidi ya moja. Kusomewa vitabu kuna auni katika kujifunza Kijerumani.

Kuna mipango mbalimbali kwa vituo vya malezi ya watoto na shule za msingi, kwa mfano kozi ya awali ya Kijerumani au madarasa ya kukuza lugha ya Kijerumani. Mtoto ambaye hafahamu Kijerumani vya kutosha hupata msaada. Pia kuna vituo vya ushauri vinavyotoa vidokezo na taarifa.

Kukuza Lugha ya Asili

Watoto wako wanapaswa pia kuweza kuzungumza vizuri lugha yao ya asili. Kwa kufanya hivyo, wataweza pia kujifunza lugha nyingine kwa urahisi zaidi. Kupitia lugha ya asili, watoto hujifunza mengi kuhusu utamaduni na mila ya nchi yao ya asili. Katika akraba nyingi, wazazi wote huzungumza lugha moja. Katika akraba nyingine hali ni tofauti. Katika hali hiyo, kila mzazi anapaswa kuwasiliana na mtoto kwa lugha yake ya asili. Mnaweza kuwasomea vitabu, kuimba nyimbo, na kucheza michezo pamoja na watoto mara kwa mara. Mnaweza pia kuwasiliana na wanafamilia kwa simu.

Katika miji mikubwa mara nyingi kuna vituo vya malezi ya watoto vyenye lugha mbili au shule za kimataifa. Mabalozi na vyama mbalimbali hutoa mafunzo ya masomo ya lugha ya asili kwa watoto wa shule. Watoto hujifunza kusoma na kuandika kwa lugha ya asili. Wanapata pia taarifa kuhusu aushi na mila ya nchi yao ya asili. Katika baadhi ya majimbo kuna pia masomo ya lugha ya asili katika shule za kawaida. Masomo haya huitwa masomo ya nyongeza ya lugha ya mama (MUE).

Mtandaoni kuna fursa nyingi, kwa mfano vikundi vya michezo kwa watoto, vilabu vya michezo, au matembezi ya pamoja. Kwa njia hii, watoto na wazazi wanaweza kutumia lugha yao ya asili mara kwa mara katika mazingira tofauti pia.

Vidokezo vya Malezi kwa Lugha Nyingi

  • Kuona lugha kwa mtazamo chanya hurahisisha kujifunza.
  • Nina na abu wanapaswa kuwasiliana na watoto kwa lugha yao wenyewe.
  • Mkiwa chengoni,zungumzeni kwa lugha ya asili.
  • Usiwalazimishe watoto kuwasiliana kwa lugha fulani. Wakati mwingine watoto hawana hamu ya kuzungumza. Watatumia lugha wanayoipendelea. Hali hii inaweza pia kubadilika tena.
  • Auni watoto kujifunza Kijerumani pamoja na lugha ya asili.
  • Vituo vya ushauri vinapeana msaada na mwongozo.Kwa maelezo zaidi, tafuta mtandaoni maneno kama "kituo cha ushauri wa kitamaduni“ au "kituo cha ushauri wa lugha nyingi“. “.

Viungo muhimu

Tufuatilie