Upatikanaji wa haraka :

Nenda moja kwa moja kwenye maudhui (Alt 1) Nenda moja kwa moja kwenye ngazi ya kwanza ya urambazaji (Alt 2)

Wanawake katika filamu
Wanawake watengenezaji wa filamu kutoka Tanzania wanasonga mbele

Kutoka Imani Mani

HAKUNA shaka, filamu ni sehemu ya dunia ya Sanaa, ikiwa njia inayotumia ubunifu katika kuiwasilisha sanaa hiyo. Ingawa Tanzania haina tasnia iliyojizatiti, kama ilivyo Hollywood, Bollywood au hata Nollywood; bado ni sehemu ya dunia hiyo. Licha ya kuwa katika hatua ya awali ya maendeleo kuliko magwiji hawa, lakini bado ingalipo. Ipo, japokuwa kwa kiasi kikubwa ni ulingo ambapo wengi miongoni mwa watendaji wake ni watu waliojiajiri wenyewe.

Ni faraja kusema kwamba suala hili halijawazuia Watanzania kuwa tayari katika kukabiliana na changamoto hiyo. Lipo tumaini kwamba siku moja nchi hii ya Afrika Mashariki itakuwa na tasnia iliyoshamiri ya filamu. Hadi kufikia wakati huo, litakuwa ni jambo lenye manufaa kwa wanawake wa nchi hii kutambuliwa kikamilifu kutokana na mchango wao muhimu wa kipekee wanaotoa katika fani hii.
Katika filamu ya T-Junction iliyotengenezwa na Amil Shivji na iliyoshinda tuzo katika vipengele kadhaa, Fatima, mhusika aliyeigizwa na Hawa Ally, anawasukuma Maria, Magdalena Christopher, katika kiti-mwendo baada ya kukutana bila ya kutarajia hospitalini. Cece Mlay alikuwa Mwongozaji Msaidizi wa filamu hii ya mwaka 2017. Katika filamu ya T-Junction iliyotengenezwa na Amil Shivji na iliyoshinda tuzo katika vipengele kadhaa, Fatima, mhusika aliyeigizwa na Hawa Ally, anawasukuma Maria, Magdalena Christopher, katika kiti-mwendo baada ya kukutana bila ya kutarajia hospitalini. Cece Mlay alikuwa Mwongozaji Msaidizi wa filamu hii ya mwaka 2017. | © Kijiweni production
Hali kama hii ya kutarajia sana matokeo mazuri ilijitokeza wakati wa mazungumzo na Priscilla Mlay, ambaye ni Mtaanzania wa kwanza kuwa Mwongozaji Msaidizi. Anafahamika kwa jina maarufu la Cece Mlay na amewahi kushika nafasi za mtu wa Kusimamia Mwendelezo na Mavazi, pamoja na nafasi ya Mwangalizi wa Muhtasari wa Filamu. Mwanamke huyu kijana aliendesha pia warsha mbili, mwaka 2017 na 2018, kwenye Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF).

Kwa njia mahsusi kabisa, warsha hizi ziliangazia masuala ya wanawake waliopo katika utengenezaji wa filamu, jambo analokiri kuwa ni fursa kubwa kwa watengenezaji wa filamu kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki kukutana na kushirikishana mawazo. Zaidi sana, warsha hizi zilikuwa kama “kifungua macho” kwake, kwani zilitoa jukwaa kwa wanawake wanaotoka ukanda huu kupata   uelewa bora zaidi wa ugumu na changamoto zinazowakabili, kwa kuzingatia shauku na mazingira yao yanayofanana.

“Ilikuwa vizuri kukutana na watu wenye fikra za uelekeo mmoja, pamoja na maono yanayofanana, wote wakipiga hatua kuelekea lengo lilelile. Nilipata msukumo wa ziada ulioniongezea nguvu. Tulifanana katika maono na mtazamo wa kutaka tasnia machachari ya filamu katika nchi zetu na katika ukanda huu,” alitamka.

Ingawa kuna wanawake watengenezaji wa filamu wa Kitanzania wenye vipaji sana, Cece Mlay anasema, mara nyingi wanakumbana na kikwazo cha nafasi ambayo wazalishaji wa filamu wa kiume wanafikiria ndipo mahali ambapo wanawake wanastahili kuwepo, ambayo kwa kiasi kikubwa ni nafasi ya uigizaji. Kuna msukumo mdogo kwa wanawake kuingia katika nyanja za kiufundi, kama vile kamera, sauti au taa.

“Endapo wazalishaji wa filamu wangetoa nafasi kwa wanawake wengi zaidi kuingia katika nyanja hizo, wangeendelea sana. Ni nadra pia kwa wanawake wa Kitanzania kuonekana katika nyanja za Maarifa Mepesi,  kama vile mameneja wa Madhari au Uzalishaji. Hata hivyo, kwa kipindi cha miaka kadhaa tumeshuhudia kasi ya mafanikio miongoni mwa wanawake wanaochukua zaidi majukumu ya uongozaji na uandishi,” anatamka.

Kuona filamu ya Binti iliyotengenezwa na Seko Shamte, ikishinda kipengele cha filamu bora kwenye tamasha la mwaka huu la ZIFF na filamu fupi ya Esther Mndeme, Salama, ikiwa katika orodha, hakika inatoa tumaini kuwa wanawake watengenezaji wa filamu wa Kitanzania wamegundua hitaji la kuongea kwa sauti zao wenyewe. Ndiyo, huyu ni yuleyule Esther Mndeme, aliyeshinda filamu fupi bora mwaka 2018, kupitia Leah, kwenye ZIFF. Wapo pia Godliver Gordian na Hawa Ally, ambao kila mmoja alishinda kipengele cha Mwigizaji Bora wa Kike, mwaka 2016 na 2017 mtawalia, kwenye ZIFF.
Esther Mndeme anapokea tuzo ya Mwongozaji Bora wa Kike, kwenye Tamasha la Kitanzania la Filamu Zetu (SZFF), kupitia mfululizo wa sinema za televisheni, Safari Yangu mwaka 2019. (Picha na Ochu Kiota) Esther Mndeme anapokea tuzo ya Mwongozaji Bora wa Kike, kwenye Tamasha la Kitanzania la Filamu Zetu (SZFF), kupitia mfululizo wa sinema za televisheni, Safari Yangu mwaka 2019. (Picha na Ochu Kiota) | © Ochu Kiota
Kuna umuhimu wa kutambua, licha ya uigizaji, Hawa Ally  pia amewahi kushika nafasi za mtu wa Kusimamia Mavazi na Mwendelezo, pamoja na Mwongozaji Msaidizi. Kila nafasi katika mpangilio wa filamu, anasema, ina safari yake yenyewe na humpatia raha kubwa sana kuwa sehemu ya timu, kugeuza hadithi za hapa nyumbani kuwa sinema za kutazamwa na wengi.

“Kuna mengi sana ya kuchunguza katika filamu, ambayo siyo lazima kuyafanikisha kutokea mbele ya kamera. Siridhishwi na uigizaji pekee. Navutiwa sana na safari niliyopitia, kuanzia katika utafiti hadi hatua ya kuoneshwa kwa filamu,” anakiri Hawa Ally.

Filamu ndefu elimishi, Softie, ya mtengeneza filamu wa kike toka Kenya, Toni Kamau, ilitia fora kwenye tamasha la mwaka huu la ZIFF na Tamasha la Filamu la Sundance la huko Texas nchini Marekani. Ni mwanamke kijana kuliko wote miongoni mwa watengenezaji wa filamu elimishi kutoka Afrika kuwahi kuwa mshirika katika taasisi inayoitwa Academy for Motion Pictures Arts and Sciences - Kitivo cha Filamu Elimishi, mkupuo wa mwaka 2020. Pia, mwongozaji wa filamu Hawa Essuman kutoka Kenya naye pia amekuwa akivuma sana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. 

Ilikuwa bahati kukutana na Profesa Martin Mhando, Mkurugenzi wa ZIFF na mhadhiri, kutoka Chuo Kikuu cha Murdoc nchini Australia. Anakiri kwamba idadi wa wanawake katika uongozaji au uzalishaji wa filamu nchini Tanzania ni ndogo sana. Hata hivyo, anapendekeza kuwa ni sharti msisitizo wa sasa uwe kwenye maandalizi ya mazingira katika jamii na katika tasnia yenyewe, yatakayowezesha kutambuliwa kwa dosari hii. Wanaume kuwa na sauti inayotawala katika filamu, anasema, itaishia kwa dunia kuwa maskini zaidi.
Wakufunzi wa Uigizaji katika warsha ya matumizi ya kamera, kwenye Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) la mwaka huu, wakichukua kumbukumbu ya matukio. Kutoka kushoto kwenda kulia ni Salome Richard (Ubelgiji), Seko Shamte na Lillian Sundqvist (Tanzania), na Marie Vermeiren (Ubelgiji). Wakufunzi wa Uigizaji katika warsha ya matumizi ya kamera, kwenye Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) la mwaka huu, wakichukua kumbukumbu ya matukio. Kutoka kushoto kwenda kulia ni Salome Richard (Ubelgiji), Seko Shamte na Lillian Sundqvist (Tanzania), na Marie Vermeiren (Ubelgiji). | © Supro
Aligusia programu ya ZIFF inayojitegemea kikamilifu kwa jina la Women Panorama (Taswira ya Wanawake). Katika programu hiyo msisitizo umewekwa kwa wanawake katika jamii, ukiangazia na kuongelea masuala yanayofaa ya jinsia, afya na jamii. Imekuwa njia ya mawasiliano ya “Nguvu na Hali ya Kuonekana kwa Wanawake” na kwa kawaida hujumuisha mfululizo wa warsha, semina na makongamano.

Inaratibiwa na kujikita kwenye suala la kuonekana kwa wanawake katika, na kupitia njia ya mawasiliano ya sinema, Sanaa na vyombo vya habari. Filamu bunilizi na filamu elimishi, juu ya masuala mahsusi ya wanawake zinakuwa nyenzo, katika programu hii.

“Duniani kuna uelekeo mmoja pekee wa maono unaosikika, yaani ule wa mwanaume kuwa mkuu wa familia au ukoo. Licha ya suala hili, kumekuwa hata hivyo na filamu zilizotengenezwa na wanawake, ambao wametambua kwamba sauti zao ni muhimu na wameendelea kwa makusudi kutoa sauti imara dhidi filamu kuendelea na mtazamo wa dunia, mtazamo wa mwanaume kuwa mkuu wa kaya, ili kuleta uwiano wa jinsi inavyopaswa kuonekana katika filamu,” anahitimisha Profesa Mhando.

MWISHO!
 

Juu