Ununuzi Madukani
Katika miji yote, na pia katika baadhi ya vijiji nchini Ujerumani, kuna masoko makubwa ya rejareja. Hapo unaweza kupata bidhaa zote muhimu kwa matumizi ya kila siku kama vile mkate, nyama, matunda na mboga, maziwa na mtindi, chokoleti, dawa za usafi, karatasi za msalani na kadhalika. Maduka nchini Ujerumani yana masaa tofauti ya kufungua. Masoko makubwa ya rejareja kawaida hufunguliwa kuanzia saa moja asubuhi hadi angalau saa mbili usiku.
Maduka na Biashara za Kawaida
Je ungependa kununua vyakula vitokavyo shambani siku hiyo? Katika maeneo mengi, mara moja au mbili kwa juma kuna gulio. Mara nyingi hufanyika siku ya Jumamosi. Katika gulio unaweza kupata matunda na mboga safi pamoja na vyakula asilia vya eneo hilo. Nyama na soseji safi hupatikana kwenye masoko au katika maduka ya nyama yaitwayo Metzgereien kusini mwa Ujerumani. Mkate safi unaweza kununua kwenye maduka ya mikate.
Maduka ya mikate, nyama na maduka mengine madogo hufungwa mapema katika miji midogo na vijijini au hufunguliwa kwa saa chache tu kwa siku.
Gulio hufanyika kawaida kuanzia macheo hadi mchana. Jumapili maduka yote hufungwa. Ni maduka ya mikate, maduka yaliyo ndani ya vituo vya reli na vituo vya mafuta tu ambayo mara nyingi huwa wazi siku za Jumapili na sikukuu.

Huduma ya Uwasilishaji
Je soko kubwa la rejareja lipo mbali sana? Au hutaki kutoka nje kwenda kufanya ununuzi? Unaweza kutumia huduma ya uwasilishaji. Kisha mja ataleta chakula hadi nyumbani kwako. Tafuta kwenye mtandao kwa kubonyeza maneno „Lieferservice Lebensmittel“ na jiji lako. Kawaida unajaza fomu kwenye mtandao. Pia masoko mengi ya rejareja yanatoa huduma za uwasilishaji. Hata hivyo huduma hii hugharimu zaidi kuliko kununua dukani. Pia kuna huduma za uwasilishaji zinazotoa vyakula vilivyopikwa tayari. Hapa unaweza kupiga simu au kuagiza kupitia mtandao.
Rejesho
Nchini Ujerumani kuna ada ya rejesho kwa makopo ya vinywaji, chupa za plastiki na chupa nyingi za glasi. Unalipa kiasi kidogo cha pesa kwa ajili ya kopo ya chupa. Kwa kawaida ni kati ya senti nane hadi ishirini na tano. Unarejeshewa pesa hizo unaporudisha vyombo hivyo vitupu dukani.
Kawaida kwenye masoko au maduka ya vinywaji kuna mashine za kuchukua chupa na makopo yaliyotumika. Unapewa stakabadhi ambayo unaonyesha kwenye kaunta. Kisha unapewa pesa yako. Chupa za glasi zisizo na rejesho huzirudisha kwenye kontena maalum za glasi.

Maduka Maalum na Mtandao
Iwapo ungependa kununua kabati, tarakilishi au jozi la viatu, unaweza kwenda kwenye jumba la biashara au duka maalum. Majumba ya biashara huwa na bidhaa nyingi tofauti tofauti. Majumba haya hupatikana hasa mijini. Maduka maalum huwa yamebobea katika bidhaa fulani. Kwa mfano kuna maduka ya samani, maduka maalum ya vifaa vya kielektroniki au maduka ya viatu. Saa za kufungua kwa kawaida huwa kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa mbili usiku, wakati mwingine hadi saa kumi na mbili unusu jioni tu.
Leo hii bidhaa nyingi pia unaweza kuzipata kupitia kwa mtandao. Mara nyingi utasubiri siku chache tu na bidhaa huletwa hadi nyumbani kwako.
Leo hii bidhaa nyingi pia unaweza kuzipata kupitia kwa mtandao. Mara nyingi utasubiri siku chache tu na bidhaa huletwa hadi nyumbani kwako.
Ununuzi wa Bidhaa za Mitumba
Unaweza pia kununua bidhaa zilizotumika tayari nchini Ujerumani kwa mfano nguo, vifaa vya elektroniki, fanicha, vitabu na mengine mengi. Mara nyingi bidhaa hizi huwa nafuu zaidi.
Mwishoni mwa wiki kuna masoko ya bidhaa za mitumba hasa katika miji mikubwa. Pia kuna maduka ya mitumba ambayo yanaongezeka kwa kasi. Tafuta tu mtandaoni kwa maneno soko la bidhaa za mitumba au bidhaa za mitumba pamoja na jiji lako.
Pia kupitia kwa mtandao unaweza kupata bidhaa zilizotumika na kwa bei ya ahueni. Hata hivyo tahadhari maadamu si punguzo zote ni za kuaminika. Majukwaa maarufu ni kama vile

Malipo
Nchini Ujerumani njia mbalimbali za malipo hutumika. Kwa pesa taslimu au kadi ya benki (ambayo pia huitwa kadi ya EC) unaweza kulipia karibu kila mahali. Ukifungua akaunti ya benki au akiba utapewa kadi ya benki au kadi ya debit na mara nyingine pia kadi ya mkopo (MasterCard au Visa). Katika baadhi ya masoko makubwa, majumba ya biashara na maduka maalum unaweza kulipa kwa kutumia kadi ya mkopo. Malipo kwa simu janja pia ni jambo la kawaida nchini Ujerumani.
Kwenye mtandao hulipwa kwa kutumia kadi ya mkopo au kadi ya debit pia kwa kukatwa pesa kutoka kwa benki au kwa ankara. Ikiwa ungependa kulipa kwa njia ya benki lazima uweke taarifa zako za akaunti mtandaoni. Kisha pesa hukatwa moja kwa moja kutoka kwenye akaunti yako. Ukipewa ankara utalipa kwa kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti yako. Kuna njia nyingine za malipo kwa mfano PayPal. Taarifa zaidi zinapatikana kwenye maandiko kuhusu Fedha na Kodi.

Bei, Dhamana na Kubadilisha Bidhaa
Katika maduka mengi nchini Ujerumani bidhaa zote huwa na bei ya kudumu. Gulioni na kwa bidhaa za thamani kubwa katika maduka maalum unaweza kubehiana. Lakini si kawaida kufanya hivyo.
Umenunua kitu na kimeharibika? Kwa bidhaa mpya una haki ya kupata dhamana ya miaka miwili unapewa bidhaa mpya. Au unarudisha bidhaa iliyoharibika na kurejeshewa pesa yako. Au unalipa kidogo zaidi. Kwa bidhaa za mkono wa pili, kipindi chake ni miezi kumi na miwili. Wakati mwingine kuna pia dhamana kwa bidhaa. Ikiwa bidhaa kwa mfano runinga: ikiharibika ndani ya kipindi cha dhamana itakarabatiwa bure. Au utapewa runinga mpya. Kipindi cha dhamana ni kuanzia miezi kumi na miwili hadi ishirini na minne tangu tarehe ya kununua bidhaa hiyo.
Ikiwa hukuridhika na bidhaa hiyo na hujaanza kuitumia unaweza kubadilisha na nyingine. Mara nyingi pia unaweza kuirudisha. Utarejeshewa pesa yako. Kubadilisha au kurudisha bidhaa kunaruhusiwa kawaida ndani ya siku kumi na nne. Hapa ni sharti uonyeshe stakabadhi ya malipo au ankara. Mara nyingi bidhaa za punguzo maalum haziwezi kubadilishwa.

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
Andika kwenye mtandao jina la duka unalohitaji na jiji lako. Pia unaweza kwenda kwenye tovuti www.gelbeseiten.de. Andika kwenye kisanduku cha "Was" kwa mfano "Supermarkt", "Fleischerei", "Bäckerei" au "Kaufhaus". Andika kwenye kisanduku cha "Wo" mahali unapoishi, kwa mfano "Köln" au "Hultrop". Kisha utaona orodha ya maduka.
Kwa kawaida bidhaa huwa na bei nafuu zaidi katika maduka makubwa kuliko yale madogo. Iwapo ungependa kuokoa pesa, ni bora kununua katika maduka ya punguzo. Chakula cha bei nafuu pia hupatikana kwenye gulio. Katika maduka mengi pia kuna punguzo maalum. Matunda na mboga huwa nafuu zaidi yanapotoka hapa Ujerumani au wakati wa msimu wake. Pia kuna maduka ya bidhaa zilizotumika na masoko ya vitu vya zamani. Huko unaweza kupata nguo za mkono wa pili kwa bei nafuu, samani zilizotumika na vifaa vingine vya nyumbani. Pia mtandaoni mara nyingi hupatikana bidhaa za bei pungufu kama vile nguo, vifaa vya umeme au samani, kwa mfano kwenye “eBay” au “Kleinanzeigen”. Fuata vidokezo vya ununuzi salama katika machapisho Broschüre „Willkommen in Deutschland“.
Katika duka la vifaa vya ujenzi. Huko utapata kila kitu unachohitaji kwa ajili ya ukarabati. Mara nyingi pia kuna samani, mimea na bidhaa za nyumbani.
Katika baadhi ya maduka makubwa, maduka maalum na maduka ya vifaa vya ujenzi. Maduka haya mara nyingi hutoa huduma ya kuwasilisha mashine nyumbani, lakini huduma hiyo inaweza kusababisha ongezeko la gharama. Au unaweza kutafuta mtandaoni. Mashine za kufua nguo zilizotumika hupatikana kwenye magazeti au kwenye tovuti. Mara nyingi mashine hizo unapaswa uzikusanye mwenyewe.
Mara nyingine ni vigumu. Baadhi ya bidhaa hazipatikani hapa. Katika miji mikubwa mara nyingi kuna maduka yenye bidhaa kutoka nchi mbalimbali duniani. Pia supermarket kubwa mara nyingi huwa na bidhaa za kimataifa. Unaweza pia kununua chakula cha kimataifa mtandaoni.
Kwa kawaida hapana. Katika miji mikubwa mara nyingi kuna duka la vyakula karibu na kituo kikuu cha reli. Vinywaji unaweza kununua kwenye vibanda. Pia vituo vya mafuta huuza vinywaji na vyakula. Vituo vya mafuta na vibanda mara nyingi huwa wazi hadi usiku wa manane. Mikate mingi huuzwa Jumapili hadi mchana. Huduma za kuleta chakula nyumbani pia zinapatikana Jumapili na usiku.
Sio kila punguzo mtandaoni ni ya kuaminika. Huna uhakika? Usitoe taarifa zako za benki. Katika brosha "Willkommen in Deutschland" (Sura ya Ununuzi) utapata vidokezo vya usalama wakati wa ununuzi wa mtandaoni.
Je, bidhaa ilikuwa na hitilafu wakati ulipoinunua? Kama ndiyo, una haki ya dhamana ya miaka miwili: unaweza kupewa bidhaa mpya, kurudisha ile yenye hitilafu na kurejeshewa pesa zako, au kulipia kiasi kidogo zaidi. Kama uligundua hitilafu miezi 6 baada ya kununua, itabidi uthibitishe kuwa hitilafu hiyo ilikuwepo tangu pale mwanzo.
Taarifa muhimu kuhusu mikataba ya ununuzi inapatikana katika brosha "Willkommen in Deutschland". Ikiwa kuna changamoto, unaweza kupata msaada kutoka kwa Kituo cha Wateja. Kwenye ukurasa wa mwanzo bonyeza jimbo lako. Utapata kiungo cha vituo vya ushauri au huduma za ushauri.
Katika duka la dawa za kuosha hupatikana bidhaa za utunzaji wa mwili, bidhaa za nyumbani au bidhaa za afya ambazo hazihitaji maagizo ya daktari. Mara nyingi pia unaweza kununua vyakula au bidhaa za asili.
Duka la dawa linauza hasa dawa na tembe za matibabu ambazo mara nyingi huhitaji maagizo ya daktari.
Duka la dawa linauza hasa dawa na tembe za matibabu ambazo mara nyingi huhitaji maagizo ya daktari.
Vyakula vya kawaida ni kama mkate wa aina mbalimbali, nyama ya nguruwe, ya ng’ombe na ya kuku, samaki, matunda na mboga mbalimbali, tambi, mchele, viazi, choroko na kunde, vitunguu na vitunguu saumu, sukari, chumvi na pilipili, maziwa ya ng’ombe na bidhaa zake kama vile krimu, siagi, jibini, mtindi au mtindi mzito, vinywaji kama maji ya chupa, sharubati, kahawa au chai, n.k. Utapata mapishi mengi mtandaoni, kwa mfano hapa:
Unarudisha makopo na chupa za matumizi mara moja na za matumizi mara nyingi katika supermarket au maduka ya vinywaji. Tofauti kati ya matumizi haya mawili yanaonekana kupitia alama na maandishi “Einweg” au “Mehrweg” kwenye chupa au makopo. “Einweg” ina maana kuwa chupa hutumika mara moja tu halafu hurejelewa. Chupa za “Mehrweg” hutumika hadi mara 25, na zile za glasi hadi mara 50. Baada ya hapo, chupa hizi hujazwa tena. Malipo ya “Einweg” ni senti 25 kwa kila chupa. Kwa “Mehrweg” kiasi hutofautiana.
Taarifa zaidi utazipata kutoka kwenye Kituo cha Wateja:
Taarifa zaidi utazipata kutoka kwenye Kituo cha Wateja: